UKAMATWAJI NYARA ZA SERIKALI KATAVI WAKITHIRI,WENGINE WAWILI WADAKWA NA KUSHIKILIWA NA POLISI,BAADHI YA WAKAZI KATAVI WATOA YA MOYONI.


Na.Issack Gerald-Mpanda,Katavi
Jeshi la polisi Mkoani Katavi,linawashikilia watu watatu baada ya kukamatwa wakiwa na vipande 12 vya meno ya tembo vikiwa na uzito wa kilogramu 11 ambapo thamani yake ni  shilingi Milioni miamoja na ishirini(120,000,000).

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa jana 29.12.2015 majira ya saa 4:00 usiku  huko mtaa wa Airtel kata ya Uwanja wa ndege tarafa ya Kashaulili Wilaya ya Mpanda.
Amewataja waliokamatwa kuwa ni  Bathromeo Augustino (26) mkazi wa Uwanja wa ndege,Geofrey Exavery (40) mkazi wa Uwanja wa ndege na Elias Mwelala (42) mkazi wa makanyagio.
Kamanda Kidavashari,amesema kuwa kukamatwa kwa watu hao, kumetokana na taarifa za raia wema kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kubainisha waharifiu walipo na hatimaye kuwatia mikonnoni mwa polisi.
Watuhumiwa wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la polisi kwa hatua za upelelezi na wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anaendelea kuwaonya wananchi kuachana na biashara haramu za nyara na uwindaji wa wanyama pori kwani ni uhalibifu wa  rasilimali za Taifa na mazingira kwa ujumla. Aidha, hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya wote wasiotii sheria.
Hata hivyo baadhi ya wakazi Mkoani Katavi wamesema kuwa kuna haja ya kuchunguza wasimamizi wa hifadhi nchini kwani hakuna nyara za serikali zinazoweza kupatikana na kuelekea hatua ya kuuzwa bila wao kufahamu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA