MTAFARUKU BAINA YA MANESI NA WANANCHI WANAOHITAJI HUDUMA HOSPITALINI MLELE.


Na.Suzan Kanenka-Mlele
Upungufu wa Manesi(wauguzi) katika kitengo cha huduma ya afya ya uzazi katika hospitali ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi,umezua mtafaruku baina ya wahudumu wa kitengo hicho na wananchi wanaostahili huduma hiyo.

Mtafaruku huo umetokea jana majira ya saa tano asubuhi katika Hospitali ya Wilaya ya Mlele kutokan na idadi kubwa ya akina mama ambayo ilijitokeza kupata matibabu kuzidi kiwango kitendo ambacho kilisababisha wananchi hao kuanza kulalamika wakidai kuwa hawapati huduma kwa wakati.
Muuguzi aliyekuwa akitibu wagonjwa katika hospitali hiyo Bi.Matha amesema kuwa kilichosababisha kutokea kwa vurugu ni kutokana na mlundikano wa akina mama na watoto.
Aida amesema kuwa mlundikano wa kazi alizokuwa nazo pia zimechangia kusababisha kutokea kwa mtafaruku huo.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mlele Bi.Lucy Kafumu amekiri kupokea taarifa hiyo ambapo amesema kuwa hali hiyo imetokana na upungufu wa watumishi katika hospitali hiyo ambapo ameiomba serikali kuongeza nguvu zaidi katika kuajiri watumishi wa kutosha katika Halmsahauri zilizopo pemezoni mwa mji.
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ina jumla ya zahanati 21 vituo vya afya 3,amabpo vinahitaji watumishi wapatao 305  huku walipo wakiwa 170 wakati huo watu 154,000 ambapo watumishi wanaohitajika wakiwa 205.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA