WAKAZI MPANDA WAASWA KUJENGA NYUMBA BORA KUJIKINGA NA MVUA ZA ELNINO


Na.Issack Gerald-MPANDA
WAKAZI wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, wameshauriwa kujenga nyumba bora ili kuepukana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua zinazosadikika kuwa za elnino.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa wilaya  ya Mpanda Bw. Paza Mwamlima wakati akizungumza na viongozi mbali mbali,  wakiwemo watendaji wa vijiji, wenyeviti wa mitaa, viongozi wa dini pamoja na viongozi wa vyama vya siasa.
Amewataka kila mmoja kwa nafasi yake awajibike kuhamasisha wananchi kuwa makini na kuwa tiba ya elnino ni nyumba bora.
Wakati huo huo, amewaomba wahandisi kujenga mitaro mitaro bora ya kupitisha maji ili maji yawe na mwelekeo mzuri na kuepusha athari kwa watu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA