RAIA WAPYA KAMBI YA KATUMBA WAENDELEA KUFURAHIA KUWA WATANZANIA


Na.Issack Gerald-MPANDA
MKUU wa makazi ya Katumba yaliyopo wilayani Nsimbo mkoani Katavi  Bw. Athuman Igwe, amesema jumla ya wakimbizi waishio katika wilaya hiyo ni elfu kumi na tisa elfu mia saba sabini na tatu, na waliopata uraia ni sitini na mbili elfu huku walio na vyeti ni hamsini na saba elfu.

Ametoa takwimu hizo jana wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA ofisini kwake. Amesema kuwa, walio na uraia wanaweza kwenda mikoa yeyote kwa uhuru hapa nchini na kwa ambao hawajapata vyeti utaratibu unafanyika.
Wakazi wa kata ya Katumba kijiji cha Mnyaki wameelezea furaha yao tangu kupata uraia wa Tanzania, na kuwaomba Watanzani kutoa ushirikiano kwao ili kuleta maendeleo katika jamii.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA