WAKAZI KATAVI WAHIMIZWA USAFI


Na.Issack Gerald-MPANDA.
Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia usafi wa Mwili Mazingira na Vyakula ili kujikinga na Maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Wito huo umetolewa na Kaimu afisa Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Noah Pius wakati akizungumza  na P5 TANZANIA MEDIA
Amesema jamii inatakiwa kunywa maji safi na salama yaliyochemshwa na kuchujwa pamoja na kuyahifadhi katika chombo kisafi.
Aidha amesema wameunda kamati ya afya ya Wilaya kwa ajili ya  kutembelea maeneo yote yanayozunguka Halmashauri hiyo kukutana na kamati za afya za vijiji pamoja na kata ili kuhamasisha jamii kuzingatia usafi. 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA