UZINDUZI MATUMIZI YA MIZANI,TAASISI ZA SERIKALI NA BINAFSI ZAASWA KUHAMASISHA MATUMIZI YA VIPIMO HALALI KATIKA BIASHARA



Mmoja wa wakazi wa Mpanda akionesha kauli mbiu ya hapa kazi tu siku ya uzinduzi wa wakala wa vipimo katika viwanja vya soko la Buzogwe Manispaa ya Mpanda (PICHA na Issack Gerald)

Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanal Issa Seleman Njiku akimkabidhi mzani mfanyabiashara mdogo kama ishara ya kuzindua matumizi ya mizani Mkoani katavi yaliyofanyika leo katika viwanja vya soko la Buzogwe (Picha Issack Gerald)

Kikao cha wakala wa vipimo na waandishi wa habari,katikakati ni Irene John Kaimu meneja wa Sehemu ya elimu habari na mawasiliano wa wakala wa vipimo kutoka makao makuu Dar Es salaam,Mwenye T-shirt Nyekundu ni Moses Ezekiel Ntungi,Mratibu wa Programu ya Ukopeshaji mizaniaMkoani Katavi  na aliyevaa koti ni Abnery Amos Nzaga Meneja wa Mkoa wakala wa vipimo Rukwa na Katavi (PICHA NA Issack Gerald)

Baadhi ya wafanyabiashara katika uzinduzi wa matumizi ya vipimo(mizani) katika biashara (PICHA na Issack Gerald)

Na.Issack Gerald-MPANDA
Taasisi binafsi na serikali ziwemo taasisi za dini,na vyombo vya habari zimeaswa kuhamasisha jamii kutambua matumizi ya mizani katika biashara ili kupata tija katika shughuli za kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bw.Issa Njiku wakati wa uzinduzi wa matumizi ya vipimo halali katika biasaha katika soko la Buzogwe lililopo Manispaa ya Mpanda.

Kwa upande wa Mratibu wa Prigram ya ukopeshaji mizani Mkoani Katavi Moses Ntungi na Irene John ambaye ni Kaimu Meneja wa sehemu ya elimu,habari na Mawasiliano wameataka wafanyabiashara na wakulima Mkoani Katavi Kutumia vipimo ili kuondokana na umaskini.
Mkoa wa Katavi umekuwa mkoa  wa kwanza kupewa kipaumbele cha uzinduzi wa uuzaji na ununuaji wa bidhaa kwa kutumia vipimo kutokana na kuwa na sifa kubwa ya kuzalisha mazao mengi ya kibiashara na vyakula.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA