KAKESE,MWAMKURU WATAHADHARISHWA KIPINDUPINDU WAASWA KUDUMISHA USAFI


Na.Issack Gerald-MPANDA.
WANANCHI wa Kata ya Kakese na Mwamkulu katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia usafi ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Afisa Afya wa kata ya Kakese na Mwamkulu Abel Joseph Paul amesema  elimu imetolewa kwa wananchi wa kata hizo juu ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kwa kuzingatia kanuni na taratibu za usafi wa mwili, vyakula na mazingira.
Aidha amesema pamoja na Wanafunzi katika kata za Kakese na Mwamkulu kuelimishwa juu ya maambukizi ya ugonjwa huu, Walimu hawana budi kuhamasisha zaidi, ukilinganisha  na msimu huu wa Matunda kama maembe.
Hata hivyo,Mkuu wa Wilaya ya MLele Bw.Suleman Isaa Njiku,akizungumza leo wakazi wa Manispaa ya Mpanda wakati wa uzinduzi wa matumizi ya vipimo au mizani katika biashara,amesisitiza kila Mkazi Mkoani Katavi kuhakikisha usafi wa kutosha unafanyikaambapo amesema kuwa yeyote amabaye atakutwa akiishi mazingira machafu atachukuliwa hatua kwa mjibu wa sheria zinavyoelekeza.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA