MKURUGENZI APEWA AGIZO KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA SOKO LA BUZOGWE


Na.Issack Gerald-MPANDA
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda amepewa siku moja kuhakikisha anafika soko la Buzogwe kuchunguza changamoto za ukosefu wa umeme,ulinzi wa biashara na maji zinazowakabili wafanyabiashara waliopo katika soko hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bw.Issa Njiku kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,baada ya kupokea taarifa ya changamoto za wafanyabiashara wa soko la buzogwe kutoka mwenyekiti wa Soko hilo Bw.Ramadhani Kalata.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa soko hilo Bw.Ramadhani Kalata amesema licha ya kutoa ushuru wa Shilingi laki moja na themanini kwa kila mfanyabiashara kila mwaka,wamekuwa wakikosa mazingira safi ya kufanyia biashara na huduma nyingine zikiwemo umeme na maji.
Kwa upande wa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamezu ngumza na P5 TANZANIA MEDIA wamesema kuwa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuhusiana na Changamoto zinazowakabili sokoni hapo zitafanyiwa utatuzi.
Wfanyabiashara hao wamezitaja changamoto zilizopo sokoni hapo kuwa ni Ukosefu wa huduma ya maji,umeme,kutozwa ushuru ambao Rais Dr.John Magufuli alisema umefutwa sambamba na kukosekana kwa ulinzi wa bidhaa zao hali inayopelekea wizi dhidi ya mali zao kutokea.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA