UONGOZI SOKO KUU MPANDA WAKANUSHA KUTOZA USHURU MARA MBILI,KUTO TOA RISITI NA UNYANYASAJI


Na.Issack Gerald-MPANDA
Uongozi wa soko kuu lililopo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi umekanusha madai yaliyotolewa na wafanyabiashara wa soko hilo kuhusu kutozwa ushuru mara mbili na wasimamizi wa soko hilo.

Hayo yamebainishwa leo na mwenyekiti wa soko bwana Aman Mahela wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA wakisema kuwa hajawahi kupokea malalamiko hayo kutoka kwa mfanyabiashara yeyote kuhusu kutozwa ushuru mara mbili na kutopewa stakabadhi.
Hata hivyo Bw.Mahela amesema  ikiwa wafanyabiashara watafanyiwa vitendo hivyo ni vyema wakatoa taarifa mapema kwake ili madai hayo yashughulikiwe kwa wakati.
Wiki mbili zilizopita wafanyabiashara wa soko kuu la mpanda waliulalamika uongozi pamoja na wasimamizi wa soko hilo kwa kuwatoza ushurru mara mbili pamoja na kutowakatia stakabadhi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA