MACHINJIO YA WANYAMA MPANDA YAFUNGULIWA


 
Moja ya bucha Manispaa ya Mpanda Rikiuza nyama baada ya machinjio kufunguliwa jana


Nembo ya Mamlaka ya chakula na dawa iliyokuwa imewekwa baadaya kufungwa kwa machinjio wiki iliyopita

Watu wakipata kitoweo machinjioni leo

Mwenyekiti wa wafanyakazi wa machinjio ya Mpanda Hoteli Bw.Benezeti Kusaya akizungmza katika kikao ambacho kimefanyika leo na vijana wanaotegemea ajira ya machinjio akihamasisha zaidi kufanyika usafi mara kwa mara

NA.Issack Gerald-MPANDA
Machinjio ya wanyama yaliyopo kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda yaliyokuwa yamefungwa na Mamlaka ya chakula na dawa Tanzania TFDA kutokana na uwepo wa  uchafu na miundombinu mibovu katika machinjio hayo yamefunguliwa.

Wakizungmza na Mpanda Radio Vijana na wafanyabiashara  wanaofanya shughuli mbalimba katika Machinjio hayo wameishukuru TFDA kwa kufungua machinjio hayo.
Wakati huohuo mwenyekiti wa wafanyakazi machinjioni Bw.Benezeti Kusaya amewasisitiza wafanyakazi wote kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha mazingira yote yanakuwa safi ili kuepuka kufungiwa tena sambamba na kusababisha mlipuko wa ugonjwa kipindupindu.
Machinjio ya Mpanda Hoteli yalifungwa wiki iliyopita na mamlaka ya chakula na dawa TFDA kufuatia kuwepo mazingira machafu na  miundombinu mibovu inayohatarisha afya ya mlaji.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA