Posts

Showing posts from 2018

MWANAMKE ASIYEJULIKANA ATUPA MTOTO WA UMRI WA SIKU 1 KATIKA UWANJA MICHEZO

Mtoto wa jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa na umri wa   siku 1 ameokotwa akiwa hai katika uwanja wa Azimio   Halmashauri ya manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi baada ya kutupwa   na mwanamke ambaye mpaka sasa hajafahamika majina wala makazi yake. Mashuhuda wa tukio wakilaani tukio hilo,wamesema mtoto huyo inasadikiwa alitupwa Ijumaa ya Juni 8 mwaka huu majira ya mchana mpaka alipookotwa majira ya saa kumi   jioni . Hata hivyo wananchi wilayani Mpanda wamesikitishwa na tukio hilo na kuomba   hatua kali zichukuliwe dhidi ya mwanamke atakayebainika kutenda unyama huo dhidi ya mtoto asiyekuwa na hatia. Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii manispaa Redgunda Mayorwa amethibitisha kupokea taarifa za mtoto huyo ambapo amesema jeshi la polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kumpata na kumfikisha katika vyombo vya sheria mwanamke aliyetenda unyama huo. Aidha ametoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali na jeshi la Polisi kuhusiana n...

BASI LAUA LAJERUHI MKOANI RUKWA

MTOTO mwenye umri wa miaka minne amefariki dunia papo hapo baada ya basi lenye Namba za usajili  T178 DHD lililokuwa likisafiri kutoka Kabwe wilayani Nkasi kuelekea mjini Sumbawanga mkoani Rukwa kuacha njia na kupindukaa huku abiria 25 wakijeruhi na tisa kati yao wakiwa ni majeruhi. Akizungumzia tukio hilo afisa mtendaji wa kata ya Kabwe  Jofrey Kuzumbi alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana Mei 5 majira ya saa 12 asubuhi katika eneo la Malimba katika kata hiyo ya Kabwe. Alisema gari hilo lilikua limebeba  abiria 43 na waliojeruhiwa ni 25 na kati yao tisa ni mahututi na wamekimbizwa katika hospitali teule ya wilaya Nkasi huku wengine wakipelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa kwa matibabu zaidi kutokana na majeraha waliyoyapata. Alisema baada ya ajali hiyo kutokea mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Beatrice Nyansio (4) alifariki papo hapo huku mzazi wake akipata majeraha. Afisa mtendaji huyo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa basi hilo n...

MSITU WA TONGWE MAGHARIBI WENYE SOKWE ZAIDI YA 800 SASA MIKONONI MWA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA

Image
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Muhando akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katuma(PICHA NA Issack Gerald) Sokwe moja ya wanyama wanaopatikana msitu wa Tongwe Magharibi Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Kapanga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Mpanda Salehe Muhando(Hayupo pichani)(PICHA NA Issack Gerald) Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Muhando,amesema wizara ya maliasili na utalii imekubali msitu wa Tongwe Magharibi kumilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kutoka katika mamlaka ya wizara hiyo. Muhando amebainisha hatua hiyo kupitia mikutano ya hadhara katika vijiji vya Kapanga na Katuma Kata ya Katuma lengo likiwa ni kuelimisha kutunza msitu huo wenye zaidi ya sokwe 800 kwa ajili ya faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA KIFO CHA MARIA NA CONSOLATA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameungana na Watanzania kuomboleza msiba wa watoto Maria na Consolata,waliofariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya mkoa wa Iringa. Rais Magufuli katika ukurasa wake wa Twitter ametuma ujumbe akielezea kusikitishwa kwake na msiba wa watoto hao ambao hivi karibuni aliwatembelea walipokuwa hospitali ya Muhimbili wakipatiwa matibabu hivi karibuni. Vifo hivyo vimetokea siku chache baada ya kuruhusiwa kutoka Hospotali ya Taifa Muhimbili ambako walikuwapo zaidi ya miezi miwili wakipatiwa matibabu. Taarifa kutoka Hospitali mkoani Iringa zinaeleza kuwa watoto hao walifariki kwa muda tofauti ambapo mmoja alifariki saa 1 usiku na mwengine alifariki saa 3 usiku. Maria na Consolata ambao ni pacha walizaliwa hapa nchini wakiwa wameungana na wakaishi hadi kujiunga na chuo kikuu wakiwa bado wameungana. Pacha hao waliokuwa na umri wa miaka 22 wamekuwa wakitunzwa na watawa wa kanisa Katoliki tangu na baada ya kuza...

ASASI ZA KIRAIA ZAINGILIA KATI SUALA LA KUONDOLEWA WALIMU WA ELIMU MAALUMU SHULENI AZIMIO

Image
Asasi za kiraia Mkoani Katavi zimelazimika kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ili kuzungumza naye kuhusu hatua ya kuwaondoa walimu waliokuwa wakifundisha watoto wenye ulemavu katika Shule ya Msingi Azimio bila kuweka wengine mbadala. Asasi hizo zimesema katika kipindi cha mwaka 2015 mpaka sasa wanafunzi wenye ulemavu hawafundishwi masomo inavyotakiwa baada ya walimu watatu kati ya watano wa elimu maalumu waliokuwepo kuondolewa katika shule hiyo na kupangiwa majukumu mengine. Zimesema,walimu watatu walioondolewa shuleni walipandishwa madaraja kuwa walimu wakuu katika shule zisizokuwa na watoto wenye ulemavu,mwingine akipandishwa daraja na kuwa mratibu elimu maalumu katika Manispaa ya Mpanda ambapo mpaka sasa amebaki mwalimu mmoja anayefundisha darasa la kwanza mpaka la saba. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu amesema hakuwa na taarifa ya kuondolewa kwa walimu hao...

NKASI KINARA WA MIMBA KWA WANAFUNZI MKOANI RUKWA

Afisa serikali za mitaa mkoani Rukwa Bw.Albinus Mgonya amesema halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani humo ndiyo inayoongoza kwa wanafunzi kupata ujauzito mkoani Rukwa. Mgonya amebainisha hali hiyo kupitia kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi katika halmashauri hiyo. Katika kipindi cha miezi tisa jumla ya wanafunzi 74 wamekatiza masomo kutokana na kupata ujauzito ambapo kwa mjibu wa katika takwimu hiyo,wanafunzi 36 ni wanafunzi wa shule za msingi na wanafunzi 38 wa sekondari waliopata ujauzito huo kuanzia Julai mwaka jana mpaka Aprili mwaka huu. Alisema kulingana na takwimu hizo,wanafunzi wanaopata ujauzito ni sawa na kuwa kila mwezi wanafunzi   wanne wa shule za msingi   wanapata ujauzito sambamba na wanne wa sekondari wanapata ujauzito. Kutokana na hali hiyo,Mgonya ameiagiza halmashauri ya wilaya Nkasi kuandaa taarifa itakayoainisha idadi ya Watoto wenye mimba,mahali walipo wazazi   wao ikiwa ni pamoja na viongozi wa maeneo yao hasa Watendaji wao wa ...

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

Image
Abdulrahman Kinana alizaliwa mwaka 1952 mkoani Arusha Arusha Kaskazini mwa Tanzania. Kinana ni mwanasiasa aliyeshika nyadhifa mbalimbali serikalini. Alihitimu shahada yake katika Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani akibobea kwenye masuala ya mikakati. Alikuwa Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa ,naibu Waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimatafa na Waziri wa ulinzi. Kinana aliwahi kufanya kazi na Jeshi la wananchi la Tanzania kwa miaka 20 kabla ya kusaafu akiwa na cheo cha ukanali mwaka 1972. Abdulrahman Kinana pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Afrika mashariki mwaka 2001 mpaka mwaka 2006. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WAKAZI WILAYANI TANGANYIKA WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Kaimu   Afisa wa Afya wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Bw.Philipo Mihayo amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugojwa wa kipindupindu kwa kufanya usafi wa   chakula na mazingira yote yanayowazunguka. Bw.Mihayo amesema ni vema   kuchukua tahadhari kwani mikoa jirani ya Rukwa na kigoma inaripotiwa kukubwa kadhia hiyo. Aidha Mihayo ametoa wito kwa wananchi kuchimba vyoo vya kisasa lakini pia kuhakikisha wanatumia maji safi na salama huku wanaokadi maelekezo akisema watachukuliwa hatua. Wilaya jirani ya Sumbawanga iliyopo Mkoani Rukwa ilitangaza kuwa katika kipindi cha Mei 11 mpaka 24 watu 7 walikuwa wamefariki dunia huku wengine 166 wakiugua ugonjwa wa kipindupindu na 44 mpaka kufikia Mei 25 walikuwa wakiendelea kupatiwa matibabu. Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya  Vibrio cholerae  zinazosababisha kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya kupikia  mchele ambapo bakteria hao walitambuliwa mwaka  1854  . Habari zaid...

BARABARA YA MPANDA-TABORA SASA RUKSA KWA MAGARI YOTE

Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mhuga hatimaye ametangaza rasmi kuwa magari yote makubwa kwa madogo yanaruhusiwa kusafiri kwa kutumia barabara ya Mpanda --Tabora kupitia Mto Koga wilayani Mlele Mei 30,2018. Kwa mjibu wa Bw.Aman   Mwakalebela ambaye ni Afisa Mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu SUMTRA amesema hali ya barabara hiyo ni nzuri na inaruhusu magari ya aina zote kupita. Hata hivyo Mwakalebela amewataka abiria waliotoa nauli ya mzunguko wa barabara kupitia Kigoma au Mbeya kwa ajili ya kwenda Tabora kudai kurejeshewa kiasi cha   nauli iliyozidi kiwango cha fedha kutoka Mpanda-Tabora na kusafiri kwa gharama halisi. Mei 26 mwaka huu Mkuu wa mkoa wa katavi Meja Jenerali Mstaafu Rapahael Muhuga alitangaza kuruhusu magari yasiyozidi tani 3 huku ukarabati wa barabara hiyo ukiendelea. Aprili 14 mwaka huu,Muhuga alitanagaza kuifunga barabara hiyo kutokana na kujaa maji katika daraja la mto koga hali iliyokuwa ikihatar...

WASAINI MKATABA ILI KUANZA UJENZI HOSPITALI YA MKOA WA KATAVI

Serikali ya Mkoa wa Katavi na Shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa SUMA JKT wamelitiana saini mkataba kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ghorofa moja la hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Katavi. Kaimu katibu tawala Bw.Wilbrod Malandu akizungumza wakati wa kutiliana saini hiyo ofisini kwake,amesema Bodi ya Zabuni imemtunuku zabuni SUMA JKT kutekeleza ujenzi wa ghorofa hilo kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 9 na milioni 798.76 ambapo ghorofa hilo litakuwa na vitanda 76 kwa safu ya chini na 71 kwa safu ya juu. Aidha Malandu amesema eneo la ujenzi wa Hospitali hiyo lenye ukubwa wa ekari 243 linapatikana Kata ya Kazima ambapo zaidi ya shilingi milioni 468 zimetumika kuwalipa fidia kwa watu 108 ili kupisha ujenzi huku zaidi ya shilingi milioni 722 zikilipwa kwa mshauri mwelekezi   Y and P Architects Tanzania Limited aliyetekeleza taarifa mbalimblai ikiwemo upembuzi yakinifu,andiko la mradi na uainishaji wa athari za kijamii na mazingira. Kwa upande wake Naibu Mkuru...

ZAIDI YA SHILINGI MIL.9 ZATUMIKA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE KATAVI

Image
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu wilayani Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu wilayani Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) Mratibu wa Mradi wa elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Fortunatus Raphael amesema mradio huo unaosimamiwa na shirika la IFI,umetumia zaidi ya shilingi milioni 9 kukarabati miundombinu ya shule za msingi Nyerere,Shanwe na Kivukoni katika kipindi cha mwaka 2017/2018. Raphael amebainisha hayo katika taarifa yake kwa wajumbe wa kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu wilayani Mpanda,kupitia kikao ambacho kimefanyika katika Ofisi za mradi huo mjini Mpanda. Aidha Raphael amesema   Mradi umetoa msaada wa mafuta maalumu kwa ajili ya watu wenye ualbino 44 wakiwemo 25 wa Manispaa ya Mpanda na 19 Halmashauri ya Nsimbo pamoja na kugawa mavazi pia baiskeli kwa watu wenye ulemavu wa viungo. Amesema muda wowote wanatarajia kuwahudumia watoto wenye ulemavu kwa mkoa...

MAHAKAMA KUU YAMWACHIA HURU DIWANI WA CCM KATA YA KATUMBA

Mahakama kuu kanda ya Sumbawanga Mkoani Rukwa ,imemwachia huru diwani wa kata ya Katumba halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mh.Senetor Baraka(ccm) miezi sita baada ya kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka sita jela. Katika mahojiano na P5TANZANIA LIMITED Mh.Baraka amesema mahakama kuu kanda ya Sumbawanga imemwachia huru mei 18 mwaka huu baada ya kukata rufaani na mahakama kujiridhisha kuwa hana hatia. Hata hivyo amesema kuachiwa kwake huru kusihusishwe na msamaha wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.John Pombe Magufuli. Mwezi Novemba mwaka 2017,mahakama wilayani Mlele Mkoani Katavi ilimhukumu senator Baraka kutumikia kifungo cha miaka sita kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mfugaji wa ng’ombe katika kata ya Katumba ili amruhusu achungie mifugo katika eneo lililozuiliwa na mahakama. Mapokezi ya diwani huyo yamefanyika katika Kijiji cha Msaginya Getini njiapanda ya kwenda Tabora na Mnyaki Katumba. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MANISPAA YA MPANDA YATANGAZA KUUWA MIFUGO

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Michael Francis Nzyungu ametangaza kuwa kuanzia Aprili 25 mwaka 2018 itakuwa ni oparesheni ya kuuwa mifugo inayozurura ovyo mitaani hususani Mbwa. Katika taarifa yake mahususi kwa ajili ya Oparesheni hiyo itakayofanyika eneo lote la manispaa ya Mpanda,amewataka   wafugaji wote katika Manispaa hiyo kufungia mifugo yote ikiwemo Ng’ombe, mbuzi, Kondoo, nguruwe na mbwa. Katika Manispaa ya Mpanda imekuwa hali ya kawaida mifugo kuzurura ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika kuharibikiwa na mazao au mali za nyumbani. Tangazo la Mkurugenzi linakuwa na aina yake kwa kuwa mara nyingi imezoeleka maonyo ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakitolewa na Maafisa watendaji wa mitaa,kata na mitaa bila mafanikio ambapo zaidi wamekuwa wakipigwa faini wenye mifugo.   Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com  

RADI YAUA MWANAFUNZI RUKWA

MWANAFUNZI wa darasa la pili shule ya msingi Kipundu James Kandege (8) amefariki dunia baada ya kupigwa radi juzi jioni akiwa nyumbani kwao na wenzake. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisa mtendaji wa kijiji cha Mabatini kata ya Namanyere Ibrahimu Adriano alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi jioni majira ya saa 10 alipokuwa ameketi nyumbani na wenzie walipokuwa wakila chakula cha mchana. Alisema kuwa marehemu akiwa na wenzie sambamba na waza zi wake wakila chakula katika kitongoji cha Katowa kijiji cha Mabatini walipigwa na radi wakiwa ndani ya nyumba yao na mwanafunzi huyo alifariki dunia papo hapo huku wengine wakisalimika. Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kipundu Josephat Laban athibitisha kutokea kwa kifo cha mwanafunzi huyo ambapo alisema kuwa shule hiyo iliwaruhusu Wanafunzi wote walishiriki katika msiba huo sambamba na mazishi huku akidai kuwa shule imempoteza mtu muhimu. Diwani wa kata ya Namanyere Evarist Mwanisawa alisema kuwa Mwanafunzi huyo alikua ni mka...

AACHIWA MKE KWA LAKI 8 BAADA YA KUFUMANIWA

MKAZIwa kijiji cha Ntumba kilichpo wilayani Tanganyika katika mkoa wa Katavi,Charles Sabuni (37)  amepwa  viboko 30 hadharani baada ya kushikwa ugoni na mke wa jirani yake Ntema Mwiwela,juzi usiku wa manane kijijini hapo. Kwa mujibu wa Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa adhabu hiyo  alipewa mgoni huyo ili iwefundisho kwake na  kwa wanaume wengine wenye tabia kama hiyo. Akisimulia tukio hilo mwenyekiti wa Kitongoji cha Ntumba Samwel Mbuya alisema lilitokea saa tisa usiku, juzi nyumbani kwa Mwiwela ambaye anaishi jirani na Sabuni. Akifafanua alisema kuwa mchana wa siku hiyo ya tukio hilo Mwiwela alimuaga mkewe kuwa ana safiri ambapo alirejea nyumbani kwake ghfla usiku wa manane na kumkuta Sabuni akiwa amelala chumbani kwake. “Mwenye mke alimthibiti mgoni wake huyo asitoroke huku akimwamuru apige mayowe huku akisema anaomba msaada kwani amefumaniwa na mke wa mtu ….. kele hizo ziliwaamsha wanakijiji wenzake ambao walikimbilia eneo la tukio n...

RAIS MAGUFULI ATEUA MWENYEKITI BODI YA WAKURUGENZI BENKI YA POSTA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt.Edmund Bernard Mndolwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania ( TPB ). Kwa mjibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,Ikulu Gerson Msigwa,Uteuzi wa Dkt.Mndolwa umeanza tarehe 23 Aprili, 2018. Dkt.Mndolwa anachukua nafasi ya Prof.Lettice Rutashobya ambaye amemaliza muda wake. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com   

WANANCHI NSIMBO WAOMBA KUBORESHEWA HUDUMA YA MAJI DIWANI AKATAA KUWEKA WAZI MIPANGO

Wananchi wa kijiji cha Mtakuja kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wameiomba serikali kushughulikia miundombinu ya huduma ya maji kijijini hapo ili wananchi waondokane na tatizo la kutofanya shughuli za maendeleo kwa sababu ya kupoteza muda mrefu wkifuatilia maji. Wamesema serikali imekuwa ikisema itaongeza mabomba ya maji ambapo mpaka sasa hakuna mipango inayotekelezwa kadri siku zinavyosonga mbele licha ya viongozi mbalimbali wakiwemo Mbunge wa Nsimbo na Diwani wa kata hiyo kutoa ahadi. Mwenyekiti wa kijiji cha Mtakuja Daud Peter Nyasio amekiri hali ya huduma ya maji katika kijiji hicho kuwa mbaya ambapom amesema visima viwili vilivyopo havikidhi idadi ya wananchi zaidi ya elfu tatu wa kijiji hicho wanaotakiwa kuapa maji. Hata hivyo Reward Sichone ambaye Diwani wa Kata ya Kapalala inayojumuisha vijiji vya Mtakuja,Songambele na Kapalala ameiambia Mpanda Radio kuwa hana jambo lolote la kuzungumza na chombo cha habari kuhusu suala la maji katika kata ya Kapal...

ACT-WAZALENDO KATAVI WATOA MAAZIMIO MIGOGORO YA ARDHI KATAVI

Chama cha ACT-Wazalendo mkoani Katavi kimeazimia kuishinikiza serikali kuchukua hatua za utatuzi wa migogoro ya ardhi inayowakabili  wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi. Joseph Mona ambaye ni Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo mkoani Katavi akizungumza katika mkutano wa chama hicho amesema kikao hicho kilichofanyika jana kililenga kufanya tahimini ya namna ambavyo serikali ya mkoa inavyoshughurikia migogoro ya ardhi inayoendelea kufukuta. Mona ametaja baadhi ya kero za wananchi zimetokana na serikali kuchukua baadhi ya maeneo yaliyokuwa makazi ya wananchi kwa madai kuwa maeneo hayo   yalikuwa katika hifadhi za misitu. Aidha Mona ametaja baadhi ya maeneo yenye migogoro kuwa ni pamoja na vijiji vya Litapunga,Luhafwe,Sitalike,Ugalla, Kanoge na Mpanda Ndogo. Hivi karibuni Chama cha ACT-Wazalendo wakiwa wameambatana na viongozi wa kijiji cha Sitalike pamoja na wananchi wa kijiji cha Sitalike walifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu R...

MGANGA MKUU JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA

MHAKAMA ya  Wilaya ya  Mpanda  Mkoani  Katavi   imemuhukumu mganga mkuu wa  Zahanati ya  Kasekese  Wilaya ya  Tanganyika  Martin  Mwashamba  (27)kifungo cha  miaka  30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la mbaka na kumpa  mimba  wanafunzi wa  dasasa la  sita  wa  shule ya  Msingi  Kasekese mwenye  umri wa miaka 15  jina  lake limehifadhiwa. Hukumu  hiyo ilitolewa  jana   na   Hakimu  mkazi wa  Mahakama ya  Wilaya hiyo  Odira  Amwol   baada ya  Mahakama  kuridhika  na  ushahidi  uliotolewa  Mahakamani  hapo  na   upande...

TRA KATAVI KUHAKIKI TIN NAMBA

Image
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoani katavi,imeanza kuhakiki namba za utambuzi(TIN NAMBA) kwa wafanya biashara waliosajiliwa katika biashara zao. Meneja wa TRA mkoani Katavi Enos Mgimba amesema zoezi la uhakiki hili ambalo limeanzia leo Aprili 18,2018 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda baadaye litaendshwa katika maeneo mengine ya Mkoa. Mgimba ametaja baadhi ya faida ya utambuzi wa TIN   NAMBA kwa TRA kuwa ni pamoja na mamlaka kuwa na taarifa sahihi za wafanyabiashara ili hali kukusanya mapato na kusaidia katika utatuzi wa changamoto mbalimbali za kibiashara. Baadhi ya wafanyabiashara ambao wamefika katika zoezi hilo wamesema zoezi hilo lina faida kwao ikiwemo kutambulika katika biashara anayoifanya. Halmashauri 5 za Mkoa wa Katavi zinazotakiwa kufanyiwa uhakiki ni Manispaa ya Mpanda na Nsimbo zinazopatikana Wilayani Mpanda,Mlele na Mpimbwe zinazopatikana Wilayani Mlele na ,Mpanda inayopatikana Wilayani Tanganyika. Kwa mjibu wa Meneja Enos Mgimba,Jumla ya wafany...

WASITISHA SAFARI ZA KUSAFIRISHA ABIRIA KATAVI KWENDA MIKOANI

Miongoni wa wafanyabiashara wa usafirishaji abiria mjini Mpanda wamesitisha huduma kutokana na ubovu wa miundombinu. Hayo yamebainishwa na baadhi ya wahudumu wa kampuni za usafirishaji wanaomiliki mabasi ya mikoani ambazo zinatumia barabara inayoanzia Mpanda kuelekea Tabora tabora. Magari yaliyokuwa yakitumia barabara ya Mpanda-Tabora yamepewa utaratibu wa kutumia barabara ya Mpanda-Kigoma au Mpanda-Mbeya ambapo wafanyabiashara wengine wamesema wanalazimika kuongeza nauli kwa shilingi elfu kumi hadi elfu kumi na tano kwa kila safari kwa kuwa umbali wa safari umeongezeka Hata hivyo kwa mjibu wa wasafirishaji hao wamesema barabara mbadala ya kupitia Uvinza Mkoani Kigoma nayo haipo katika hali nzuri kitendo kinachosababisha ugumu wa safari. Jumamosi ya Aprili 16,2018,mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Rafael Muhuga alitangaza kufungwa kwa barabara ya Mpanda-Tabora baada ya barabara hiyo kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Mwishoni mwa wiki iliyopia mku...

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MPYA WA VIONGOZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Magufuli leo Aprili 15,2018 amefanya uteuzi wa Majaji 10 wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali,Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka,Wakili Mkuu wa serikali na Naibu Wakili Mkuu wa serikali. Aidha,Dkt.Magufuli amesema amefanya uteuzi huo wa Majaji wa Mahakama Kuu kwa lengo la kujaza nafasi za Majaji waliostafu na amefanya uteuzi wa Wakili Mkuu wa serikali na Naibu wake kwa lengo la kuhakikisha ofisi za Mwanasheria Mkuu wa serikali,Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Mkuu wa serikali zinafanya kazi vizuri zaidi katika kushughulikia masuala ya Mahakama. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com    

DOKTA TITUS KAMAN ADAIWA KUMTELEZA MWANAMKE KATAVI BAADA YA KUMZALISHA MTOTO MWENYE ULEMAVU

Mwanamke mmoja ambaye amejitambulisha kwa jina la Bi.Amina Salumu mkazi wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi amedai Dkt.Titus Kamani ambaye amewahi kuwa kiongozi mkubwa hapa nchini amemtelekeza mwanamke huyo baada ya kuona amejifungua mtoto mwenye ulemavu. Bi.Amina Salumu ametoa malalamiko hayo leo Aprili 14,2018 katika uwanja wa Azimio Mjini Mpanda kupitia mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi. Kwa mjibu wa Mwanamke huyo,Titus Kamani mbunge aliyeko Dodoma kwa sasa amewahi kuwa Dkt.Mkuu katika Hospitali ya Reft Valley pia mbunge Mkoani Mwanza ambapo. Mbali na mwanamke huyo wanawake wengine wamedaiwa kutelekezwa,kutishwa maisha na waume waliowazalisha huku wengine wakinyimwa matumizi muhimu ya kifamilia. Wananchi wengi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi wamejitokeza katika uwanja wa Azimio ili kueleza kero zao kwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi meja jeneral Mstaafu Raph...

BARABARA YA MPANDA—TABOARA YAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga ametangaza barabara ya Mpanda– Tabora kufungwa kwa muda usiojulikana kuanzia leo Jumamosi Aprili 14,2018. Katika picha ni gari lililosombwa na maji 2016 na kuuwa watu Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo leo katika mkutano wa hadhara ambao ameuitisha kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi kupitia mkutano amabo umeitishwa katika uwanja wa Azimio mjini Mpanda. Muhuga amesema barabara hiyo imefungwa baada ya maji kujaa barabarani kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na hivyo kuhatarisha maisha ya wasafiri. Kwa upande wake mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi Amani Mwakalebela amesem kutokana na barabara kuharibika kwa kiasi kikubwa,wenye mabasi watalazimika kusafirisha abiria kupitia mkoani Kioma au Mbeya. Mwaka 2016 barabara ya Mpanda – Tabora ilifungwa baada ya kukatika kwa daraja la mto Koga ambapo takribani watu 10 walipoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria ...

TMA WATOA TAHADHARI YA MVUA KUBWA LEO APRILI 13,2018

Image
Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania TMA imesema vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa leo Aprili 13,2018. Katika taarifa ya mamlaka hiyo ambayo imetolewa jana Aprili 12,2018 mikoa ambayo inatarajiwa kuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa ni Kagera,Geita, Mwanza,Mara, Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Tabora,Katavi,Morogoro, Ruvuma,Dar Es Salaam, Pwani, Tanga Pamoja Na Visiwa Vya Unguja Na Pemba. Aidha TMA imetoa angalizo kwa kusema kuwa Vipindi Vifupi Vya Mvua Kubwa Vinatarajiwa Katika Baadhi Ya Maeneo Ya Mikoa Ya Rukwa, Njombe, Mbeya, Iringa Na Songwe. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com

RC KATAVI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KESHO JUMAMOSI APRILI 14,2018

Image
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga kesho siku ya Jumamosi Aprili 14,2018 ameitenga kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi. Kwa mjibu wa kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi,Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na maeneo mengine ya Mkoa wa Katavi kufika katika viwanja vya Azimio Mjini Mpanda kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi ili kueleza kero zao. Muhuga amesema atasikiliza kero za wananchi wote zinazohusu masuala mbalimbali na kuzipatia majibu papo hapo. Hii ni mara ya Kwanza kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga,kusikiliza kero za wananchi katika eneo la wazi linalojumuisha wananchi wote tangu alipoteuliwa mwaka 2016 kuwa Mkuu wa Mkoa kabla ya hapo amekuwa akisikiliza kero za wananchi Ofisini kwake. Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com

RAIS MAGUFULI LEO APRILI 13,2018 KUWAVALISHA VYEO MAOFISA WA JWTZ AKIWEMO MKUU WA WILAYA YA BUHIGWE ANAYEREJESHWA JESHINI

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli leo Aprili 13,2018 anatarajia kuwavalishwa vyeo maofisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)   ambao amewapandisha vyeo jana Aprili 12,2018. Kati ya maofisa hao yumo Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali M E Gaguti ambaye sasa anapanda cheo na kuwa Brigedia Jenelari na kurejeshwa Jeshini. Kwa mjibu wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania , Jenelari Venancy Mabeyo amesema maofisa walioteuliwa wanakwenda kuimarisha safu za utendaji kazi kijeshi. ORODHA YA WALIOPANDISHWA VYEO 1.Meja Jenerali Peter Massao aliyepandishwa kuwa Luteni Jenarali. 2.Brigedia Jenerali Henry Kamunde aliyepandishwa na kuwa meja jenerali. 3.D.D.M Mullugu 4.J.J Mwaseba 5.A.S Mwamy 6.R.K Kapinda 7.C.D Katenga 8.Z.S Kiwenge 9.M.A Mgambo 10.A.M Alphonce 11.A.P Mutta 12.A.V Chakila 13.M.G Mhagama 14.V.M Kisiri 15.C.E Msolla 16.S.M Mzee 17. C.J Ndiege 18.I.M Mhona 19.R.C Ng’umbi 20.S.J Mnkande ...