NKASI KINARA WA MIMBA KWA WANAFUNZI MKOANI RUKWA
Afisa serikali za mitaa mkoani Rukwa
Bw.Albinus Mgonya amesema halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani humo ndiyo
inayoongoza kwa wanafunzi kupata ujauzito mkoani Rukwa.
Mgonya amebainisha hali hiyo kupitia
kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi katika halmashauri hiyo.
Katika kipindi cha miezi tisa jumla
ya wanafunzi 74 wamekatiza masomo kutokana na kupata ujauzito ambapo kwa mjibu
wa katika takwimu hiyo,wanafunzi 36 ni wanafunzi wa shule za msingi na
wanafunzi 38 wa sekondari waliopata ujauzito huo kuanzia Julai mwaka jana mpaka
Aprili mwaka huu.
Alisema kulingana na takwimu hizo,wanafunzi
wanaopata ujauzito ni sawa na kuwa kila mwezi wanafunzi wanne wa shule za msingi wanapata ujauzito sambamba na wanne wa
sekondari wanapata ujauzito.
Kutokana na hali hiyo,Mgonya
ameiagiza halmashauri ya wilaya Nkasi kuandaa taarifa itakayoainisha idadi ya
Watoto wenye mimba,mahali walipo wazazi
wao ikiwa ni pamoja na viongozi wa maeneo yao hasa Watendaji wao wa
vijiji na kata ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Halmashauri nyingine za Mkoa wa Rukwa
ni pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Vijijini,Nkasi, Kalambo na
Manispaa ya Sumbawanga.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments