WASAINI MKATABA ILI KUANZA UJENZI HOSPITALI YA MKOA WA KATAVI
Serikali ya Mkoa wa Katavi na Shirika
la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa SUMA JKT wamelitiana saini mkataba
kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ghorofa moja la hospitali ya rufaa ya Mkoa wa
Katavi.
Kaimu katibu tawala Bw.Wilbrod Malandu
akizungumza wakati wa kutiliana saini hiyo ofisini kwake,amesema Bodi ya Zabuni
imemtunuku zabuni SUMA JKT kutekeleza ujenzi wa ghorofa hilo kwa gharama ya zaidi
ya shilingi bilioni 9 na milioni 798.76 ambapo ghorofa hilo litakuwa na vitanda
76 kwa safu ya chini na 71 kwa safu ya juu.
Aidha Malandu amesema eneo la ujenzi
wa Hospitali hiyo lenye ukubwa wa ekari 243 linapatikana Kata ya Kazima ambapo zaidi
ya shilingi milioni 468 zimetumika kuwalipa fidia kwa watu 108 ili kupisha
ujenzi huku zaidi ya shilingi milioni 722 zikilipwa kwa mshauri mwelekezi Y and P Architects Tanzania Limited
aliyetekeleza taarifa mbalimblai ikiwemo upembuzi yakinifu,andiko la mradi na
uainishaji wa athari za kijamii na mazingira.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi mtendaji
wa Shirika la uzalishaji mali la jeshi la kujenga taifa SUMA JKT Kanali Andrew
Mkinga pamoja na kuipongeza serikali ya mkoa wa Katavi kwa kumpatia zabuni hiyo
kwa niaba ya Mkurugenzi wa SUMA JKT,ameahidi kujenga kwa weledi na kukamilisha
kazi kwa wakati uliopangwa.
Mkoa wa Katavi ulianza Mpango wa
ujenzi wa hospitali ya Rufaa tangu mwaka 2014 ambapo katika eneo la ujenzi
kunatarajia kuwemo vitengo mbalimbali vikiwemo Chuo cha sayansi na tiba,chuo
cha uuguzi na utafiti pamoja na shule,maduka,hotel, stendi ya mabasi na viwanja
vya michezo.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments