WAKAZI WILAYANI TANGANYIKA WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU
Kaimu Afisa
wa Afya wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Bw.Philipo Mihayo amewataka wananchi
kuchukua tahadhari dhidi ya ugojwa wa kipindupindu kwa kufanya usafi wa chakula na mazingira yote yanayowazunguka.
Bw.Mihayo amesema ni
vema kuchukua tahadhari kwani mikoa
jirani ya Rukwa na kigoma inaripotiwa kukubwa kadhia hiyo.
Aidha Mihayo ametoa
wito kwa wananchi kuchimba vyoo vya kisasa lakini pia kuhakikisha wanatumia
maji safi na salama huku wanaokadi maelekezo akisema watachukuliwa hatua.
Wilaya jirani ya
Sumbawanga iliyopo Mkoani Rukwa ilitangaza kuwa katika kipindi cha Mei 11 mpaka
24 watu 7 walikuwa wamefariki dunia huku wengine 166 wakiugua ugonjwa wa
kipindupindu na 44 mpaka kufikia Mei 25 walikuwa wakiendelea kupatiwa matibabu.
Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya Vibrio cholerae zinazosababisha kuhara majimaji
yenye rangi kama maji ya kupikia mchele ambapo
bakteria hao walitambuliwa
mwaka 1854 .
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments