BARABARA YA MPANDA-TABORA SASA RUKSA KWA MAGARI YOTE
Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mhuga hatimaye
ametangaza rasmi kuwa magari yote makubwa kwa madogo yanaruhusiwa kusafiri kwa
kutumia barabara ya Mpanda --Tabora kupitia Mto Koga wilayani Mlele Mei
30,2018.
Kwa mjibu wa Bw.Aman
Mwakalebela ambaye ni Afisa Mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri
wa majini na nchi kavu SUMTRA amesema hali ya barabara hiyo ni nzuri na
inaruhusu magari ya aina zote kupita.
Hata hivyo Mwakalebela amewataka abiria waliotoa nauli ya
mzunguko wa barabara kupitia Kigoma au Mbeya kwa ajili ya kwenda Tabora kudai
kurejeshewa kiasi cha nauli iliyozidi kiwango
cha fedha kutoka Mpanda-Tabora na kusafiri kwa gharama halisi.
Mei 26 mwaka huu Mkuu wa mkoa wa katavi Meja Jenerali Mstaafu
Rapahael Muhuga alitangaza kuruhusu magari yasiyozidi tani 3 huku ukarabati wa
barabara hiyo ukiendelea.
Aprili 14 mwaka huu,Muhuga alitanagaza kuifunga barabara hiyo
kutokana na kujaa maji katika daraja la mto koga hali iliyokuwa ikihatarisha
usalama wa watumiaji wa barabara.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments