BASI LAUA LAJERUHI MKOANI RUKWA
MTOTO
mwenye umri wa miaka minne amefariki dunia papo hapo baada ya basi lenye Namba
za usajili T178 DHD lililokuwa likisafiri kutoka Kabwe wilayani Nkasi
kuelekea mjini Sumbawanga mkoani Rukwa kuacha njia na kupindukaa huku abiria 25
wakijeruhi na tisa kati yao wakiwa ni majeruhi.
Akizungumzia
tukio hilo afisa mtendaji wa kata ya Kabwe Jofrey Kuzumbi alisema kuwa
ajali hiyo ilitokea jana Mei 5 majira ya saa 12 asubuhi katika eneo la Malimba
katika kata hiyo ya Kabwe.
Alisema
gari hilo lilikua limebeba abiria 43 na waliojeruhiwa ni 25 na kati yao
tisa ni mahututi na wamekimbizwa katika hospitali teule ya wilaya Nkasi huku
wengine wakipelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa kwa matibabu zaidi
kutokana na majeraha waliyoyapata.
Alisema baada ya ajali hiyo kutokea mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Beatrice Nyansio (4) alifariki papo hapo huku mzazi wake akipata majeraha.
Alisema baada ya ajali hiyo kutokea mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Beatrice Nyansio (4) alifariki papo hapo huku mzazi wake akipata majeraha.
Afisa
mtendaji huyo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa basi hilo na
baada ya ajali hiyo dereva wa gari hilo aliyefahamika kwa jina moja tu la Moses
alikimbia na mpaka sasa haijulikani alipo.
Kamanda
wa Polisi mkoani Rukwa George Kyando alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na
kuongeza kuwa bado uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea ikiwa ni pamoja na
kuendelea kumsaka dereva wa gari hilo ambaye amekimbia ili akamatwe na
kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments