MSITU WA TONGWE MAGHARIBI WENYE SOKWE ZAIDI YA 800 SASA MIKONONI MWA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Muhando akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katuma(PICHA NA Issack Gerald) |
Sokwe moja ya wanyama wanaopatikana msitu wa Tongwe Magharibi |
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Kapanga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Mpanda Salehe Muhando(Hayupo pichani)(PICHA NA Issack Gerald) |
Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Muhando,amesema wizara ya maliasili na utalii imekubali
msitu wa Tongwe Magharibi kumilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kutoka
katika mamlaka ya wizara hiyo.
Muhando amebainisha hatua
hiyo kupitia mikutano ya hadhara katika vijiji vya Kapanga na Katuma Kata ya
Katuma lengo likiwa ni kuelimisha kutunza msitu huo wenye zaidi ya sokwe 800 kwa
ajili ya faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mh.Hamadi Mapengo amesema
mchakato wa kuomba kumiliki msitu huo ulianza mwaka 2002 ambapo kwa sasa kutaongezeka
mapatao yatokanayo na msitu ikiwa ni pamoja na kupata watalii kwa ajili ya kuja
kuwaona wanyama.
Kwa mjibu wa Kaimu wa
afisa ardhi na maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elisha
Mengele,vijiji vipatavyo 11 vinavyozunguka msitu huo vinatarajia kunufaika
zaidi na msitu huo.
Amevitaja vijiji hivyo
kuwa ni Lugonesi,Lwega, Kapanga, Katuma,Mpembe,Vikonge,Bugwe,Mlibasi,Isubangala
na Kusi inayojumuisha vijiji vya Mishamo.
Hata hivyo
kinachosubiriwa sasa ni msitu huo kutangazwa katika gazeti la serikali ili
kumilikiwa rasmi na Halmashauri ya wilaya ya Mpanda.
Katika ziara hiyo
ambayo inafanyika katika vijiji vyote 11,mkuu wa wilaya alikuwa ameambatana pia na
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda,Mh.Theodora Romward
Kisesa(Diwani Viti Maalumu ccm),Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Wilayani
Tanganyika akiwa na Katibu wake Bw.Jackson huku pia mikutano hiyo ikihudhuriwa
na wenyeviti wa vijiji,mabalozi na maafisa watendaji wa vijiji.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments