TRA KATAVI KUHAKIKI TIN NAMBA
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoani
katavi,imeanza kuhakiki namba za utambuzi(TIN NAMBA) kwa wafanya biashara waliosajiliwa
katika biashara zao.
Meneja wa TRA mkoani Katavi Enos
Mgimba amesema zoezi la uhakiki hili ambalo limeanzia leo Aprili 18,2018 katika
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda baadaye litaendshwa katika maeneo mengine ya
Mkoa.
Mgimba ametaja baadhi ya faida ya
utambuzi wa TIN NAMBA kwa TRA kuwa ni
pamoja na mamlaka kuwa na taarifa sahihi za wafanyabiashara ili hali kukusanya
mapato na kusaidia katika utatuzi wa changamoto mbalimbali za kibiashara.
Baadhi ya wafanyabiashara ambao
wamefika katika zoezi hilo wamesema zoezi hilo lina faida kwao ikiwemo
kutambulika katika biashara anayoifanya.
Halmashauri 5 za Mkoa wa Katavi
zinazotakiwa kufanyiwa uhakiki ni Manispaa ya Mpanda na Nsimbo zinazopatikana
Wilayani Mpanda,Mlele na Mpimbwe zinazopatikana Wilayani Mlele na ,Mpanda inayopatikana
Wilayani Tanganyika.
Kwa mjibu wa Meneja Enos Mgimba,Jumla
ya wafanyabiashara 4000 waliopo mkoani Katavi wanatarajiwa kuhakikiwa katika
zoezi ambalo linatarajiwa kufikia tamati Aprili 27,2018.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments