MAHAKAMA KUU YAMWACHIA HURU DIWANI WA CCM KATA YA KATUMBA
Mahakama kuu kanda ya Sumbawanga
Mkoani Rukwa ,imemwachia huru diwani wa kata ya Katumba halmashauri ya wilaya
ya Nsimbo Mh.Senetor Baraka(ccm) miezi sita baada ya kuhukumiwa kutumikia
kifungo cha miaka sita jela.
Katika mahojiano na P5TANZANIA LIMITED Mh.Baraka amesema
mahakama kuu kanda ya Sumbawanga imemwachia huru mei 18 mwaka huu baada ya
kukata rufaani na mahakama kujiridhisha kuwa hana hatia.
Hata hivyo amesema kuachiwa kwake
huru kusihusishwe na msamaha wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh.Dkt.John Pombe Magufuli.
Mwezi Novemba mwaka 2017,mahakama
wilayani Mlele Mkoani Katavi ilimhukumu senator Baraka kutumikia kifungo cha
miaka sita kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mfugaji wa ng’ombe
katika kata ya Katumba ili amruhusu achungie mifugo katika eneo lililozuiliwa
na mahakama.
Mapokezi ya diwani huyo yamefanyika
katika Kijiji cha Msaginya Getini njiapanda ya kwenda Tabora na Mnyaki Katumba.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments