DOKTA TITUS KAMAN ADAIWA KUMTELEZA MWANAMKE KATAVI BAADA YA KUMZALISHA MTOTO MWENYE ULEMAVU
Mwanamke mmoja ambaye amejitambulisha
kwa jina la Bi.Amina Salumu mkazi wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi amedai Dkt.Titus
Kamani ambaye amewahi kuwa kiongozi mkubwa hapa nchini amemtelekeza mwanamke
huyo baada ya kuona amejifungua mtoto mwenye ulemavu.
Bi.Amina Salumu ametoa malalamiko
hayo leo Aprili 14,2018 katika uwanja wa Azimio Mjini Mpanda kupitia mkutano wa
hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael
Muhuga kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Kwa mjibu wa Mwanamke huyo,Titus
Kamani mbunge aliyeko Dodoma kwa sasa amewahi kuwa Dkt.Mkuu katika Hospitali ya
Reft Valley pia mbunge Mkoani Mwanza ambapo.
Mbali na mwanamke huyo wanawake
wengine wamedaiwa kutelekezwa,kutishwa maisha na waume waliowazalisha huku
wengine wakinyimwa matumizi muhimu ya kifamilia.
Wananchi wengi kutoka maeneo
mbalimbali ya Mkoa wa Katavi wamejitokeza katika uwanja wa Azimio ili kueleza
kero zao kwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi meja jeneral Mstaafu Raphael Muhuga
aliwaahidi wananchi kuwa kero zao zote zitajibiwa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments