BARABARA YA MPANDA—TABOARA YAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga ametangaza barabara ya
Mpanda–Tabora
kufungwa kwa muda usiojulikana kuanzia leo Jumamosi Aprili 14,2018.
Katika picha ni gari lililosombwa na maji 2016 na kuuwa watu |
Muhuga amesema
barabara hiyo imefungwa baada ya maji kujaa barabarani kufuatia mvua
zinazoendelea kunyesha na hivyo kuhatarisha maisha ya wasafiri.
Kwa upande wake mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi Amani Mwakalebela amesem kutokana na barabara kuharibika kwa kiasi kikubwa,wenye mabasi watalazimika kusafirisha abiria kupitia mkoani Kioma au Mbeya.

Mwaka 2016 barabara
ya Mpanda – Tabora ilifungwa baada ya kukatika kwa daraja la mto Koga ambapo takribani
watu 10 walipoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na
maji.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments