RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA KIFO CHA MARIA NA CONSOLATA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameungana na
Watanzania kuomboleza msiba wa watoto Maria na Consolata,waliofariki dunia usiku
wa kuamkia leo katika hospitali ya mkoa wa Iringa.
Rais
Magufuli katika ukurasa wake wa Twitter ametuma ujumbe akielezea kusikitishwa
kwake na msiba wa watoto hao ambao hivi karibuni aliwatembelea walipokuwa
hospitali ya Muhimbili wakipatiwa matibabu hivi karibuni.
Vifo
hivyo vimetokea siku chache baada ya kuruhusiwa kutoka Hospotali ya Taifa Muhimbili
ambako walikuwapo zaidi ya miezi miwili wakipatiwa matibabu.
Taarifa kutoka Hospitali
mkoani Iringa zinaeleza kuwa watoto hao walifariki kwa muda tofauti ambapo
mmoja alifariki saa 1 usiku na mwengine alifariki saa 3 usiku.
Maria na Consolata ambao ni pacha walizaliwa hapa
nchini wakiwa wameungana na wakaishi hadi kujiunga na chuo kikuu wakiwa bado
wameungana.
Pacha
hao waliokuwa na umri wa miaka 22 wamekuwa wakitunzwa na watawa wa kanisa
Katoliki tangu na baada ya kuzaliwa na mwaka jana walijiunga na chuo kikuu cha
Ruaha Catholic University na kuanza na masomo ya kompyuta kabla ya kuanza
masomo kamili Oktoba.
Maria na Consolata walikuwa wamefanya
mitihani yao ya mwisho ya kidato cha sita,katika shule ya Sekondari ya Udzungwa
mjini Iringa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments