MANISPAA YA MPANDA YATANGAZA KUUWA MIFUGO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Michael Francis Nzyungu ametangaza kuwa kuanzia
Aprili 25 mwaka 2018 itakuwa ni
oparesheni ya kuuwa mifugo inayozurura ovyo mitaani hususani Mbwa.
Katika taarifa yake mahususi kwa
ajili ya Oparesheni hiyo itakayofanyika eneo lote la manispaa ya Mpanda,amewataka wafugaji wote katika Manispaa hiyo kufungia
mifugo yote ikiwemo Ng’ombe, mbuzi, Kondoo, nguruwe na mbwa.
Katika Manispaa ya Mpanda imekuwa hali
ya kawaida mifugo kuzurura ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika
kuharibikiwa na mazao au mali za nyumbani.
Tangazo la Mkurugenzi linakuwa na
aina yake kwa kuwa mara nyingi imezoeleka maonyo ya mara kwa mara ambayo
yamekuwa yakitolewa na Maafisa watendaji wa mitaa,kata na mitaa bila mafanikio
ambapo zaidi wamekuwa wakipigwa faini wenye mifugo.
Comments