WASITISHA SAFARI ZA KUSAFIRISHA ABIRIA KATAVI KWENDA MIKOANI
Miongoni
wa wafanyabiashara wa usafirishaji abiria mjini Mpanda wamesitisha huduma
kutokana na ubovu wa miundombinu.
Hayo
yamebainishwa na baadhi ya wahudumu wa kampuni za usafirishaji wanaomiliki
mabasi ya mikoani ambazo zinatumia barabara inayoanzia Mpanda kuelekea Tabora tabora.
Magari
yaliyokuwa yakitumia barabara ya Mpanda-Tabora yamepewa utaratibu wa kutumia
barabara ya Mpanda-Kigoma au Mpanda-Mbeya ambapo wafanyabiashara wengine
wamesema wanalazimika kuongeza nauli kwa shilingi elfu kumi hadi elfu kumi na
tano kwa kila safari kwa kuwa umbali wa safari umeongezeka
Hata
hivyo kwa mjibu wa wasafirishaji hao wamesema barabara mbadala ya kupitia Uvinza
Mkoani Kigoma nayo haipo katika hali nzuri kitendo kinachosababisha ugumu wa
safari.
Jumamosi
ya Aprili 16,2018,mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Rafael Muhuga
alitangaza kufungwa kwa barabara ya Mpanda-Tabora baada ya barabara hiyo kujaa
maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mwishoni mwa wiki
iliyopia mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu
Sumatra Mkoani Katavi Amani Mwakalebela alikuwa amesema kutokana na barabara ya
Mpanda-Tabora kuharibika kwa kiasi kikubwa watawapatia waraka wa mwongozo wa
safari ili wenye mabasi wasafirishe abiria kupitia mkoani Kioma au Mbeya.
Mwaka 2016 barabara ya Mpanda – Tabora ilifungwa baada ya
kukatika kwa daraja la mto Koga ambapo takribani watu 10 walipoteza maisha
baada ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments