VIONGOZI WA CHAMA CHA UPINZANI WA CHADEMA WAACHIWA HURU


Wanasiasa saba wa upinzani wakiwemo viongozi wa juu wa chama kikuu cha upinzani Tanzania Chadema wameachiwa huru baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwapatia dhamana wanasiasa sita wiki iliyopita lakini waliendelea kubaki rumande kwa kuwa hawakuwepo mahakamani kukamilisha masharti ya dhamana yao.
Mtuhumiwa wa saba,Halima Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe,aliongezwa leo katika orodha ya washtakiwa na kufanya jumla ya washtakiwa kuwa saba.
Washtakiwa wote wanakabiliwa na mshtaka 8 ambayo ni pamoja na kukusanyika na kufanya maandamano kinyume na sheria pamoja na kutoa maneno yanayoweza kusababisha vurugu na chuki miongoni mwa jamii.
Kwa msingi huo,Halima Mdee pia amepatiwa dhamana kwa masharti kama yale yale ya wenzake wa awali ambayo ni pamoja na wadhamini wawili,kila mdhamini asaini bondi ya shilingi za Kitanzania milioni 20 na kukabidhi vitambulisho vinavyotambulika kisheria.
Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri anayesikiliza kesi hiyo ametaja tarehe 16 April kuwa ndio siku ya Kusikilizwa kwa awali kwa kesi ya wanasiasa hao.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA