MATUKIO YA UHALIFU NI 0 WAKATI WA SHEREHE ZA PASAKA MKOANI KATAVI


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda amesema hakuna uhalifu wowote ulijitokeza katika kipindi cha sikukuu ya pasaka.
Kamanda Nyanda amebainisha hatua hiyo wakati akizungumzia hali ya ulinzi na usalama katika sherehe za pasaka kwa mwaka 2018 ambazo wakaristo kote duniani husherehekewa sikukuu hiyo.
Aidha amesema hakuna matukio ya vifo wala majeruhi yaliyotokana na ajali za barabarani ambazo zimesababishwa na ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani.
Hata hivyo,mbali na kuwapongeza wananchi wa mkoa wa Katavi kwa kuthamini usalama na kusherehekea kwa amani na utulivu,amesema jeshi la polisi litaendelea kudhibiti viashiria vyovyote vy akiuharifu ili wananchi waendelee kuwa salama pamoja na mali zao.
Katika kipindi cha Januari mpaka Machi 2018,matukio kadhaa ya uhalifu yalitokea mkoani Katavi ikiwemo matukio ya Januari 27 kata ya Ugalla na Februari 25 mwaka huu mgodi wa Islamilomo wilayani Mpanda ambapo watu wawili walikufa kwa kupigwa risasi na majambazi nyakati za usiku katika matukio hayo huku wengine kadhaa wakijeruhiwa na mali kadhaa kuibwa.
Mbali na matukio hayo vibaka nao wamekuwa wakitajwa kuwa kero kwa wakazi wengi kutokana na wizi wa mali za majumbani hasa ukatwaji wa nyavu madirishani na kuiba mali kama vile simu,radio,tv,sola za umeme na hata komputa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA