NIDA YASEMA KUJIANDIKISHA VITAMBULISHO VYA TAIFA NI BURE


Kaimu msajili wa vitambulisho vya Taifa Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi Bi.Nasra Said amesema hakuna gharama zozote ambazo wananchi wanatakiwa kulipia ili kujiandikisha kwa ajili ya kupata kitambulisho cha taifa.
Bi.Nasra amesema wananchi wanapokwenda kujiandikisha wanatakiwa wawe na nakala mojawapo kati ya kitambulisho cha Mpiga kura,cheti cha kuzaliwa au cheti cha shule.
Badhi ya wananchi wilayani Tanganyika wakiwemo Bw.Emmanuel Adiriano na Samweli John wamelalaka kulipishwa fedha mpaka shilingi 1000 kwa ajili  ya kujiandikisha huku wengine wakisema hawana elimu yoyote kuhusu vitambulisho hivyo vya taifa na kuhofia kukosa haki yao ya msingi.
Utaratibu wa kuanzisha Vitambulisho vya Taifa kwa raia wa Tanzania na wageni waishio nchini Tanzania lilianzishwa mwaka 1968 katika kikao kilichojumuisha wajumbe Kutoka nchi za Tanzania,Kenya,Uganda na Zambia.
Kwa mjibu wa maelezo ya serikali ya Tanzania,vitambulisho hivyo vinalenga kuimarisha mahusiano ya kiusalama yanayozingatia Utawala wa Sheria katika nchi hizo nne kwa kuwapatia raia wake vitambulisho vya taifa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA