MANISPAA YA MPANDA YATANGAZA KUUWA MIFUGO


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Michael Francis Nzyungu ametangaza kuwa kuanzia Aprili 25 mwaka 2018 itakuwa ni oparesheni ya kuuwa mifugo inayozurura ovyo mitaani hususani Mbwa.
Katika taarifa yake mahususi kwa ajili ya Oparesheni hiyo itakayofanyika eneo lote la manispaa ya Mpanda,amewataka  wafugaji wote katika Manispaa hiyo kufungia mifugo yote ikiwemo Ng’ombe, mbuzi, Kondoo, nguruwe na mbwa.
Katika Manispaa ya Mpanda imekuwa hali ya kawaida mifugo kuzurura ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika kuharibikiwa na mazao au mali za nyumbani.
Tangazo la Mkurugenzi linakuwa na aina yake kwa kuwa mara nyingi imezoeleka maonyo ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakitolewa na Maafisa watendaji wa mitaa,kata na mitaa bila mafanikio ambapo zaidi wamekuwa wakipigwa faini wenye mifugo.
 Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA