WAVUVI RUKWA WAIPONGEZA ZAMBIA KUONDOA ZUIO BIASHARA YA SAMAKI


WAVUVI wa samaki katika ziwa Tanganyika wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameishukuru serikali ya Zambia kwa kuondoa marufuku ya biashara ya samaki katika nchi hiyo.
Marufuku hiyo ilikuwa imewekwa kwa takribani wiki mbili zilizopita kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu nchini humo.
Shukrani hizo wamezitoa jana na kusema marufuku hiyo ilikuwa imewaathiri kiuchumi kutokana na kuwa soko kubwa la samaki wanaovuliwa katika ziwa Tanganyika wilayani Kalambo mkoani Rukwa nchini Tanzania ilikuwa ikitegemea soko katika nchi hiyo jirani.
Mmoja wa wavuvi aliyejitambulisha kwa jina la Richard Sichone alisema serikali ya nchi hiyo imeondoa marufuku hiyo baada ya jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo kuonesha mafanikio ambapo hivi sasa wavuvi hao wameanza kuuza samaki wao nchini Zambia.
Alisema katika kipindi ambacho serikali ya nchi hiyo ilikuwa imezuia uvuvi katika nchi hiyo pamoja na biashara ya samaki kutoka nchi za Tanzania na Congo DRC kutokana na kipindu pindu walikabiliwa na ugumu wa maisha kwa kuwa walikuwa wakiuza samaki kwa bei ya hasara tofauti na walipokuwa wakiuza nchini Zambia.
Sichone alisema katika nchi hiyo kuna makampuni 12 ambayo yamekuwa yakinunua samaki tani 1,200 kila siku ambapo kilo moja wavuvi wamekuwa wakiuza kwa shilingi 5,000 za kitanzania lakini katika kipindi ambacho nchi hiyo ilipiga marufuki ya biashara ya samaki soko lilishuka ambapo walikuwa wakiuza kilo moja kwa shilingi 1,500 na kulikuwa kuna kampuni moja tu ya Premji iliyopo Kasanga ambayo ilikuwa ina uwezo wa kununua tani nane za samaki.
Naye Michael Sichilima mvuvi wa kijiji cha Kapele katika mwambao wa ziwa Tanganyika wilayani kalambo alisema kitendo ilichokifanya serikali ya Zambia ni cha kupongezwa kwani kimetoa fursa ya biashara si tu kwa wavuvi wa nchini humo lakini pia wavuvi kutoka nchi jirani watanufaika.
Hata hivyo wavuvi hao wanasema wanaheshimu sheria za nchi hiyo ili wasigeuke kuwa kero nchini humo

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA