WATU WAWILI MIKONONI MWA POLISI KATAVI KWA KUHAMASISHA MAANDAMANO

Na.Issack Gerald-Katavi
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda amesema jeshi hilo linawshikilia watu wawili wakituhumiwa kuhamasisha maandamano kwa njia ya Mtandaoni.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda
Kamnada Nyanda ametoa kauli wakati akizungumza na mtandao huu Ofisini kwake kuhusu namna ambavyo jeshi hilo limejipanga kudhibiti maandamano hayo.
Aidha Kamanda Nyanda ametoa onyo kali kwa watu watakaohamasisha au kuandamana ambapo amesema watakaoandamana watakabiliwa na hatua kali za kisheria.
Baadhi ya wananchi Mkoani Katavi wakiwemo Said Rashid Mdemela,Juma Bairon Mwanda,Jonathan John Midende,Paul Makelele na Wenseslaus Obed wamesema maandamano hayo hayana tija kwa watanzania na hawatashiriki kwa sababu ni wakati wa kufanya kazi za maendeleo na kuepuka mkono wa sheria kwa mambo yasiyokuwa na maana.
’Majina ya watuhumiwa hayakuwekwa wazi kwa sababu za kiuchunguzi na upelelezi utakapokamilika wanatarajiwa kufikishwa mahakamani’’-Alisema Kamanda Nyanda
Maandamano hayo yanayodaiwa kuratibiwa na mwanamke Mange Kimambi aliyeko nje ya nchi,yamepangwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu kuelekea Ikulu ya Rais kwa ajili ya kupinga baadhi ya mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA