RAIS MAGUFULI AFYANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA ULINZI WA ISRAEL IKULU



Mhe.Rais
Magufuli ametaka makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Israel katika
maeneo mbalimbali yakiwemo ulinzi na usalama,mafunzo na masuala ya kiuchumi
yatiwe saini haraka ili utekelezaji uanze mara moja.
Aidha,Mhe.Rais
Magufuli amemuomba Mhe.Lieberman kumfikishia ujumbe Waziri Mkuu wa Israel Mhe.Benjamin
Netanyahu wa kumualika kutembelea Tanzania na pia kuanzisha ofisi ya ubalozi
hapa nchini badala ya kutumia ofisi za ubalozi zilizopo Nairobi nchini Kenya.
Kwa
upande wake Mhe.Avigdor Lieberman amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa
kumkaribisha na kufanya naye mazungumzo na pia amemhakikishia kuwa Israel
imejipanga kuongeza uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania katika maeneo yote
ya makubaliano pamoja na kusaidia kilimo na usindikaji wa chakula.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
Comments