MAGAIDI WAWILI HATARI WA IS WAKAMATWA


Raia wawili wa Uingereza wanaodhaniwa kuwa wanachama wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislam cha IS wanashikiliwa na kundi la wapigaji wa Kikurd.
Alexanda Kotey(34) na mwenzake El Shafee Elsheikh(29) ni miongoni mwa vijana wawili waliokuwa wanasakwa kati ya wenzao ambao walikwisha kukamatwa.

Image caption
Magaidi Alexanda Kotey na El Shafee Elsheikh
Magaidi Alexanda Kotey na El Shafee Elsheikh

Kundi hili la vijana wanne kutoka raia wa Uingereza ndani ya kundi la IS walikuwa ni kundi hatari linalofahamika kama Beatles hiyo ikiwa ni kutokana na lafudhi yao wanapozungumza.

Maofisa wa Marekani wamesema kundi hilo lililokuwa likihusika na utoaji mateso pamoja na kuua ndani ya IS linadaiwa kuwachinja Zaidi ya watu 27 mateka kutoka nchi za kimagharibi na kutoa mateso makali kwa wengine wengi tu.
Hawa ni kundi hatari kwa ajili ya mauaji na mateso,ambalo lilikuwa linajumuisha watu kama Mohammed Emwazi almaarufu kama Jihadi John ambaye alikuwa akionekana katika picha za video akiwa anachinja watu.
Aliuawa katika mashambulizi ya anga mwaka 2015 katika mji wa Raqqa ngome ya zamani ya IS.
Lakini wapo pia Aine Davis ambaye naye alikuwa akitokea Uingereza,alihukumiwa baada ya kubainika kuwa alikuwa mmoja wa viongozi waandamizi wa kundi la Islamic State na alifungwa mwaka jana huko Uturuki.
Wengine wanaounda kundi hili la Beatles ni Alexanda Kotey ambaye naye anatoka London magharibi ambapo kwa mjibu wa Marekani yeye alikuwa katika kitengo cha utesaji na alikuwa mtu anayetoa usajili kwa wanaojiunga na IS.
El Shafee Elsheikh huyu yeye ni miongoni mwa waliokuwa wakiunda genge hili hawa ndiyo Beatles.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA