CHADEMA WAZUNGUMZIA KIFO CHA KADA WAKE MKONGWE


Mwenekiti wa Chadema taifa Mh.Freeman Mbowe ameeleza kusikitishwa na taarifa ya kifo cha Tambwe Richard Hizza.
Amesema kuwa Hizza alipotoka CCM na kwenda upinzani kwake yeye ni kama alikuwa anatubu kwani hakutaka kufa akiwa ndani ya CCM.
Mbowe amesema hayo jana Februari 8 baada ya kusikia taarifa ya kifo cha Tambwe Richard Hizza ambaye amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana.
Kufuatia kifo cha Hizza Mwenyekiti wa CHADEMA amedai wao ili kumuenzi kamwe hawawezi kurudi nyuma bali watasimamia yale wanayoyaamini ili kumuenzi na kufikia matamanio ambayo kiongozi huyo alikuwa akiyatamani.
Hizza katika moja ya mikutano ya Chadema
Richard Hizza amekuwa akishiriki katika kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni toka siku ya ufunguzi wa kampeni hizo Januari 27,2018 na siku moja kabla ya kifo chake alishiriki kampeni za kumnadi mgombea wa Ubunge kupitia CHADEMA. 
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA