KADA MKONGWE WA CHADEMA AFARIKI DUNIA



Mwanasiasa mkongwe na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tambwe Hizza amefariki dunia asubuhi ya kuamkia leo (Alhamis ) akiwa nyumbani kwake kwa ugonjwa wa pumu.
Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha kifo hicho akisema Hiza amefariki leo asubuhi nyumbani kwake Mbagala akiwa amelala.
Hiza amefariki kipindi ambacho alikuwa katika timu ya kampeni za kumnadi mgombea wa ubunge wa Chama hicho katika Jimbo la Kinondoni, Salumu Mwalimu na jana jioni alipanda jukwaani kumnadi.
Mwaka 2015,Hiza alitangaza kujiunga na Chadema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu akitokea CCM ambako aliwahi kuhudumu kama mkuu wa kitengo cha propaganda wa chama hicho tawala.
Kabla ya kujiunga na CCM alihama kutoka katika Chama cha Wananchi (CUF) ambako pia alihamia kutoka NCCR-Mageuzi.
Katika kampeni za urais 2015, Hiza alikuwa katika jopo la kumnadi mgombea wa Chadema aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa,Edward Lowassa na mara zote alikuwa anapanda jukwaani mwanzoni kama alivyokuwa akifanya kwenye kampeni za  Mwalimu zinazoendelea.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA