WANANCHI MKOANI KATAVI WAMEZUNGUMZIA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Na.Issack Gerald
Baadhi ya wananchi mkoani katavi wamesema ni vyema jamii kubadili tabia ikiwemo kuachana na ngono zembe ili kuweza kuepukana na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Mapema leo hii wamebainisha hali hiyo wakati wakizungumzia namna wanavyoielewa siku ya ukimwi duniani ambapo wananchi hao akiwemo Mwajuma Idd Bakary na Islam Said wamesema elimu kuhusiana na ugonjwa wa ukimwi wamekuwa wakiipata na wameweza kuwahamasisha wengine kupima afya zao.
Sanjari na hayo pia  wamewaasa vijana kuhakikisha wanapima afya zao mara kwa mara na kuwa mabalozi kwa wengine namna ya kujiepusha na maambukizi mapya ya Ukimwi.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa yenye maambukizi makubwa ya ugonjwa Ukimwi ambapo kwa miaka ya hivi karibuni Mkoa wa Katavi una asilimia 5.9.
Siku ya ukimwi duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 ya kila mwaka na kauli mbiu kwa mwaka huu inasema  “Changia mfuko wa maisha,Tanzania bila Ukimwi inawezekana”

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA