SOKO LA HALMSHAURI YA WILAYA YA NSIMBO NI CHAFU HALINA CHOO TANGU MWAKA 1975

Na.Issack Gerald
Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake miaka 40 iliyopita hali inayosababisha baadhi ya wafanyabishara kujisaidia vichakani ambopo muda wowote huenda mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ukatokea.
Hayo yamebainishwa na wakazi wa Kata ya Katumba wanaotumia soko hilo ambapo wamesema wanaishi kwa taharuki ya kukumbwa na kipindupindu kutokana na kukithiri kwa uchafu na ukosefu wa choo katika soko hilo.
Kwa upande wao mwenyekiti wa soko hilo Bw.Leonard Kigwasu na Afisa Mtendaji wa vijiji vya Mnyaki A na B Bw.Kombo Masatu wamekiri kuwepo kwa uchafu sokoni hapo huku wakisema choo kinatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi miwili ijayo.
Baadhi ya wamiliki wa maduka ya kibiashara wamesema wanatozwa kuanzia shilingi elfu sita na mia tano huku wafanyabishara wanaouzia bidhaa chini wakilipa ushuru kila wanapouza.
Kwa mjibu wa takwimu iliyotolewa hivi karibuni na Diwani wa Kata ya Katumba Senetor Braka,jumla ya vijiji 16 vya kata hiyo vyenye jumla ya wakazi zaidi ya elfu hamsini wanapata huduma ya soko hilo.
Awali soko hilo lilikuwa likiendeshwa na wakuu wa Ofisi za makazi za Shirika la wakimbizi Duniani ambapo miaka ya hivi karibuni wakazi hao walipewa uraia wa Tanzania na soko hilo kuhamishiwa katika mamlaka ya Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA