WAKAZI KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO HAWANA MAJI KWA ZAIDI YA MIEZI 6

Na.Issack Gerald
WAKAZI wa kata ya Katumba Halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wameilalamikia serikali kwa kutoshughulikia tatizo la maji kata ya katumba ambapo kwa sasa hawana maji kwa muda wa miezi 6.
Wakazi hao wametoa malalamiko hayo kwa Nyakati tofauti wakati wakati wakizungumza kuhusu tatizo la maji linalowasumbua kwa sasa ambapo wamesema limesababishwa na mashine iliyokuwa ikisukuma maji kuharibika.
Mwenyekiti wa jumuia ya watumia maji Bw.Ngeze Joel amekiri kuwepo kwa tatizo hilo akisema tatizo la maji limetokana na kuharibika kwa mashine huku Afisa Mtendaji wa vijiji vya Mnyaki A na Mnyaki B Kombo Masatu amesema baadhi ya vifaa vimenunuliwa ili kumaliza tatizo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Ndui Stesheni Hussein Nasri mahali Mashine hiyo ilipo kwa upande wake amesema hakuna mwelekeo wa lini ufumbuzi utapatikana.
Kwa mjibu wa Bw.Hussein Nasri Mashine hiyo yenye thamani ya karibu shilingi milioni 80 inasamabaza maeneo ya huduma za jamii kama soko,shule,kituo vya polisi na sehemu nyingene muhimu.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA