UTAPELI NJE YA IKULU NDOGO MKOANI KATAVI

Na.Issack Gerald
Taasisi ya  kupambana na kuzuia  rushwa TAKUKURU  Mkoani  Katavi  imewakamata watu wawili ambao walijifanya kuwa ni maafisa watasisi hiyo na kwenda kupokea rushwa ya shilingi 400,000 karibu na majengo ya ikilu ndogo. 
Watuhimiwa hao waliofahamika kwa Majina ya Nicodemo  Peter  pamoja na  Peter   Mwaninsawa  wakazi wa  Mtaa wa  Nsemlwa katika  Manispaa ya  Mpanda walijifanya maafisa wa takukuru na kutapeli fedha hizo.
Tukio hilo lilitokea  jana   majira ya saa 4 asubuhi nje ya Ikulu  ndogo ya  Mkoa wa  Katavi  iliyopo  jirani na   ofisi ya TAKUKURU.
Mkuu wa  Takukuru mkoani Katavi  John   Minyenya  amewaambia  wandishi wa  habari kuwa watuhumiwa  hao walikamatwa  kufuatia  mtego  ulioandaliwa  na  taasisi  hiyo  baada ya kupata taarifa kutoka kwa msiri wao juu ya watu hao waliokuwa wakijiita ni  maafisa wa takukuru kitengo cha  uchunguzi.
Alisema  kabla ya  kukamatwa kwa wahumiwa  hao walimpigia  simu  msiri wa takukuru  na  kujitambulisha  kuwa  wao ni maafisa wa taasisi hiyo na wanalo  jalada la uchunguzi za  huhuma   zinazo  mkabili  msiri  huyo akihusishwa na rushwa.
Hivyo walimtaka awape  kiasi cha   shilingi 400,000 ili  walifunge   jalada hilo kwa  kufuta tuhuma zinazomkabili  msiri  huyo  ambaye ni afisa mtendaji wa  Kijiji  cha  Vikonge  Wilayani Tanganyika ambaye walidai  kuwa   anatuhumiwa kwa tuhuma za  kupokea  rushwa kutoka  kwa wafugaji  ambapo alikamata  mifugo ya  wafugaji na kisha  aliiachia  baada ya kupokea rushwa ya kiasi shilingi 2,500,000.
Minyenya  alieleza msiri  huyo  ambaye   hapendi   na  anapinga  vitendo vya rushwa  alilazimika  kufika  kwenye  ofisi ya  Takukuru  na  kutoa  taarifa juu ya  maafisa  hao   bandia wa  Takukuru Ndipo   Takukuru walipoanza  kufanya  uchunguzi juu ya  malalamiko  hayo  kutokana  na  takukuru kutokuwa  na  watu  wenye  tabia  kama  hiyo ya  kuomba  na  kupokea rushwa kutoka kwa watuhumiwa.
Alisema  ndipo  walipoandaa  mtego wa kuwakamata  watuhumiwa  hao  ambao walimtaka  msiri  huyo   awapelekee  fedha  hizo   nje ya   jengo la  Ikulu  ndogo ya  Katavi kwa  kuwa  ni  jirani na  ofisi  yao ya  Takukuru  ili   iwe  rahisi wao kutoka  ndani ya   ofisi  za  Takukuru na kufika  kwenye eneo la  tukio.
Kufuatia  makubaliano  hayo ulipofika  muda wa  kupeleka   fedha hizo kwa  maafisa  hao  bandia alikwenda  kuchukua  fedha  zilizokuwa  na   namba za  takukuru na  kisha  kuwapelekea   katika  eneo  walilokuwa  wamekubaliana kwa  ajiri ya  kubabidhiana  na  mara walifika na kupokea  fedha  hizo  nje ya jengo la  Ikulu,ndipo walipokamatwa  na  Maafisa wa  Takukuru wakiwa na  fedha  hizo.
Minyenya  amesema  watuhumiwa hao  wanaendelea kushikiliwa  na  watafikishwa  mahakamani  ili kujibu  mashita  mawili  ya  kujifanya  maafisa wa  Takukuru  na shitaka la  pili likiwa ni ni  kuomba na  kupoke  rushwa.
Chanzo:Gurian wa Rukwa Kwanza Blog

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA