IGP SIRO AKIWA MKOANI KATAVI AMESISITIZA KUCHUKUA HATUA KALI ZA KISHERIA KWA WAHARIFU NCHINI

Na.Issack Gerald
Mkuu wa Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa ziarani Mkoani Katavi,amesema Jeshi la polisi litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu wote wanaojihusisha na uharifu mbalimbali ikiwemo Mauaji ya watu kwa imani za kishirikina.
IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kupokea ripoti ya mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga kuhusu hali ya ulinzi,amani na usalama mkoani Katavi.
Aidha Siro amesema uharifu Mkoani Katavi umepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na uharifu uliokuwepo katika miaka michache iliyopita.
Wakati huo huo Kamanda Sirro ambaye aliwasili jana Mkoani Katavi kwa zaiara ya kikazi ya siku mbili,ameweka jiwe la msingi ujenzi wa zahanati ya jeshi la polisi Mjini Mpanda.
Katika hatua nyingine IGP akiwa ameambatana na maafisa wa polisi kutoka makao makuu ya polisi nchini pamoja na waliopo Mkoani Katavi,amekagua na kuangalia maonesho mbalimbali ya namna jeshi la Polisi Mkoani Katavi linavyoweza kupambana na uharifu mbalimbali.
Katika mkoa wa Katavi matukio makubwa yaliyokuwepo miaka ya hivi karibuni ni pamoja na utekaji magari eneo la Magorofani Wilayani Tanganyika katika barabara ya Mpanda – Kigoma.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA