SERIKALI IMEAGIZA KUSITISHA UVUVI ZIWA RUKWA

Na.Issack Gerald
SERIKALI mkoani  Rukwa imeagiza kulifunga ziwa Rukwa kwa muda usiojulikana kutokana na shughuli za uvuvi kuchangia kasi ya ugonjwa wa kipindupindu katika ziwa hilo.
Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alitoa agizo hilo wakati akizingumza na wavuvi kwa lengo la kuwaeleza sababu za kulifunga ziwa hilo na kuzuia kabisa uvuvi kutoendelea.
Alisema baada ya kukaa na wataalamu wa afya wamekubaliana kusitisha shughuli za uvuvi kwani zimekuwa chanzo kikubwa cha kuenea ugonjwa huo. 
Alisema athari inayopatikana katika kambi hizo za uvuvi zitawaathiri walaji wa samaki wanaotokana ziwa hilo hasa waliopo Sumbawanga mjini kwani wanategemea samaki hapo Kama kutoweo na kuwataka walio waliopiga kambi katika ziwa hilo kwa ajili ya uvuvi waondoke mara moja kwani hawataruhusiwa kuingia ziwani kuendelea kuvua samaki. 
Wakati huo huo aliagiza kufunguliwa maeneo maalumu kwa ajili ya kuwatibia wagonjwa  watakaopatikana kwani wasipofanya hivyo mlipuko wa ugonjwa huo utaendelea kuongezeka na watu wengi zaidi wataendelea kupoteza maisha kwa ugonjwa huo. 
Mkuu huyo wa mkoa alifanya  ziara  katika kambi ya wavuvi ya mererani iliyopo katika kijiji cha Ilanga Kata ya Muze Wilayani Sumbawanga katika bonde la Ziwa Rukwa ambapo mpaka sasa Jumla ya wagonjwa 9 waliripotiwa kuugua kipindupindu.
Awali akitoa taarifa ya ugonjwa huo Afisa afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Plasidus Malapwa alisema ugonjwa huo ulibainika tangu novemba 23 kutokana na mgonjwa aliyetoka kambi ya Lichili Kijiji cha Lichili wilayani Momba Mkoani Songwe na kufia katika kambi ya kamchanga Kata ya Muze wilayani Sumbawanga na kuanzia hapo wagonjwa walianza kuongezeka hali iliyosababisha kuanzishwa kwa kambi nne kuzunguka ziwa Rukwa.
Naye Mganga mfawidhi wa Zahanati ya Muze Dkt Aron Mtolo alisema hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kudhibiti ugonjwa huo ikiwamo kufunga migahawa michafu 8 kuvifungia vilabu vya kuuzia pombe ambapo pia mapipa manne na debe tatu ya pombe  ilimwagwa na wanywaji pombe 14 walilipishwa faini ya shilingi 20,000 kila mmoja.
Chanzo:Gurian wa Rukwa Kwanza Blog
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA