UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA MKOANI KATAVI,ZAIDI YA WANAFUNZI 9000 WAMEKOSA NAFASI YA KUIJUNGA KIDATO CHA KWANZA MAWAK 2018

Na.Issack Gerald
Zaidi ya wanafunzi 9000 waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mkoani Katavi wamekosa nafasi ya kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2018 kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa. 
Akitangaza matokeo ya mtihani huo katika kikao maalumu cha uchaguzi wa wanafunzi Afisa Elimu mkoa wa Katavi Ernest Hinju amesema jumla watahiniwa 7,190 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kutwa.
Aidha watahiniwa 162 hawakuweza kufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali hali iliyopelekea wadau wa elimu kujadili changamoto za kushuka kwa elimu, kwani kulinganisha na mwaka uliopita mkoa wa Katavi umeshika nafasi ya 9 kitaifa kutoka nafasi ya 2 mwaka uliopita 
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Katavi Bw. Gideon Marandu amezitaka halmashauri zote kuhakikisha wanafunzi waliokosa nafasi wanapata nafasi ifikapo Februari mwaka 2018.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA