WATOZA USHURU PUNGUFU TA TANI 1 KUKIONA CHA MOTO,SERIKALI KUANZA KULIPA MISHAHARA YA WATUMISHI WA UMMA MWEZI HUU

Na.Issack Gerald
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na Usalama nchini kuwakamata watumishi na watoza ushuru wote nchini watakamtomtoza ushuru mwananchi anayesafrisha mzigo usiozidi tani moja.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati akihutubia wananchi mjini Bukoba Mkoani Kagera ambapo alikuwa na shughuli ya kuweka jiwe la msingi upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
Katika hatua nyingine,Rais Magufuli amesema kuanzia mwezi huu serikali itaanza kulipa stahiki zote za wafanyakazi wa umma wanazoidai serikali ikiwemo malimbikizo ya mishahara ambapo zaidi ya shilingi bilioni 159 zimetengwa kwa ajili hiyo.
Rais magufuli amefanya ziara mkoani Kagera kama mwendelezo wa ziara zake za kikazi katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo wiki iliyopita alifanya ziara katika mikoa ya Mwanza na Geita na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa mjibu wa rais Magufuli,keshokutwa atakwenda Nchini Uganda kwa ajili ya kwenda kuweka jiwe la msingi ujenzi wa bomba la mafuta linalojengwa kuanzia Uganda hadi Tanzania.

                       Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA