RAIS MUGABE AMEMTUMBUA JIPU MAKAMU WAKE WA RAIS

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amemfuta kazi Makamu wake wa Rais Emmerson Mnangagwa.
Emmerson Mnangagwa
Kwa mjibu wa Waziri wa Habari wa Zimbabwe Simon Kahaya Moyo,Bw.Mnangagwa (75) ameachishwa kazi kwa madai kuwa alionyesha tabia za kukosa uzalendo na uaminifu hasa kwa Rais.
Kufutwa kwake ni ishara kuwa mke wa rais Robert Muabe, Bi.Grace,atafuata nyayo za mumeme za kuwa rais wa Zimbabwe
Siku ya Jumapili Bi.Grace Mugabe alitoa wito wa kutaka mumewe amfute kazi Mnangagwa.
Bw.Mnangagwa ambaye ni mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi,amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais Mugabe.
Kufutwa kwake kunakuja baada ya Rais Robert Mugabe(93)kutishia kumuachisha kazi Bw Mnangagwa, hatua ambayo imezua uvumi kuwa anataka mke wake kuchukua hatamu za kuliongoza taifa hilo.
Akihutubia mkutano wa wanachama wa makanisa ya asili mji Harare siku ya Jumapili,Bi Mugabe alisema Bw Mugabe alimtaka Mnangagwa na wafuasi wake kumuonyesha uzalendo au afutwe kazi.
Chama cha Zanu-PF kinatarajiwa kuifanyia mabadiliko katiba yake wakati wa mkutano na kuweka nafasi mbili za makamu wa rais,nafasi moja ikiwa ni ya mwanamke.
Nafasi hiyo inatarajiwa kujazwa na Bi.Mugabe na kuongeza uwezekano wa kumrithi mume wake.

              Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA