WAKAZI MKOANI KATAVI WAMESHAULIWA KUJIUNGA NA ASASI MBALIMBALI

Wananchi mkoani Katavi wameshauriwa kujiunga na asasi mbalimbali za kimaendeleo ili kujikwamua kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Emiliana Stanslaus, mkufunzi wa asasi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Girl Guides Association wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya You Report kwa ajili ya kutoa taarifa mbalimbali kwa njia ya ujumbe mfupi.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoani Katavi  Bi Anna Shumbi amewataka wananchi kutumia fursa hiyo ili waweze kuandaa maisha yao ya baadae kulingana na dhima ya chama ya kuwainua kiuchumi

Tanzania Girl Guides Association imelenga kuwaendeleza wasichana na wanawake  katika masuala  mbalimbali ya kijamii na kiuchumi


Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA