MKOANI KATAVI DIWANI JELA MIAKA 3 KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA

Na.Issack Gerald

Mahakama ya wilaya ya Mlele imemkumu kwenda jela diwani wa kata ya Katumba Senator  Jeriti Baraka kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa.

Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Timothy Swai, mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa katavi Bahati Haule amedai mtuhumiwa alitenda kosa hilo 12.05.2016 kwa kuomba rushwa ya shilingi 500,000/=ili asimuhamishe mfugaji mmoja kwenye eneo lililozuiliwa na mahakama kuendesha shughuli za ufugaji.

Taarifa iliyotolewa na  taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani katavi imesema mtuhumiwa amehukumiwa kwa makosa mawili tofauti ambapo kosa la kwanza ni kuomba rushwa na kosa la pili ni kupokea rushwa.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kosa la kuomba rushwa mtuhumiwa amehukumiwa kutoa faini ya shilingi 500,000/= au kifungo cha miaka mitatu na kosa la kupokea rushwa mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela bila faini.

Katika taaifa ya Takukuru inaeleza kuwa baada ya taarifa kupokelewa Mei 12 mwaka 2016,uchunguzi wa awali ulifanyika kasha kuandaliwa mtego wa rushwa uliofanikisha kukamatwa kwa Bw.Senetor Jeriti Baraka katika eneo la Msaginya Getini akipokea Shilingi 400,000/=kutoka kwa mtoa taarifa ikiwa ni sehemu ya malipo y ashilingi 500,000/= kwani awali alikuwa ameshapokea shilingi 100,000/=kutoka kwa mtoa taarifa kama malipo ya awali.
Hukumu hiyo dhidi ya kiongozi huyu aliyechaguliwa na wananchi ilitolewa Juzi Novemba 20,2017.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA