SUALA LA BOMOABOMOA KATA YA SITALIKE LIMEFIKA BUNGENI

Na.Issack Gerald
Wizara ya Mali asili na Utalii imesema haina mpango wa kuruhusu shughuli za kilimo katika Kijiji cha Matandalani na Igongwe kata ya Stalike iliyopo mkoani Katavi.
Kauli hiyo imetolewa na naibu Waziri wa Mali asili na Utalii Japhet Hasunga alipo kuwa akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Nsimbo mkoa wa Katavi Richad Mbogo ambaye amehoji kwanini maeneo hayo yasi idhinishwe kisheria kwa shughuri za kibinadam.
Akijibu swali hilo amesema serikali imetenga maeneo mengine kwa ajili ya wakazi walio ondolewa katika maeneo hayo yanayotajwa kuwa hifadhi za misitu.
Katika hatua nyingine amefafanua uwepo wa mpango wa kuyapitia upya maeneo hayo ili kuona uwezekano wa kubadilisha matumizi pale itakapo onyesha ulazima huo.

Mara kwa mara mamia ya wakazi mkoani Katavi wamekuwa wakiondolewa kinguvu katika maeneo mbali mbali ya vitongoji na Vijiji kwa madai ya kuvamia misitu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA