MAHAKAMA KUU IMETENGUWA KUFUKUZWA WABUNGE 8 NA MADIWANI 2 WA CUFU



Mahakama Kuu leo imetengua kufukuzwa kwa Wabunge 8 na Madiwani 2 wa Chama cha Wananchi,CUF na kusitisha pia mchakato wa kuwafukuza uanachama mpaka shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.
Aidha Mahakama hiyo pia imemzuia Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa,Prof.Ibrahim Haruna Lipumba, Magdalena Sakaya na Bodi ya Wadhamini ya CUF kujadili kuhusu uanachama wa Wabunge na Madiwani hao.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma ya CUF Taifa, imeeleza kuwa, Mahakama Kuu imekubaliana na Hoja za Wabunge 8 wa chama hicho na imeona hoja za msingi za madai yao zinazopaswa kuangaliwa kuhusu uhalali wa masuala yote yaliyowasilishwa mbele ya Mahakama hiyo.
Imefafanua kwamba, Mahakama Kuu pia imeyatupilia mbali mapingamizi mengine yote yaliyowekwa na Prof. Lipumba na Wenzake katika shauri hilo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA