JESHI LA POLISI RUKWA:VIONGOZI WA DINI UOMBEENI MKOA WA RUKWA MAUAJI YAPUNGUWE
Na.Issack
Gerald
JESHI
la polisi mkoani Rukwa limewaomba viongozi wa dini wazidi kumuomba Mungu ili
lifanikiwe kumaliza vitendo vya mauaji ya nayotokana na imani za kishirikina
mkoni humo.

Amesema
kuwa miongoni mwa changamoto zinazoukabili mkoa wa Rukwa ni mauaji yanayotokana
na imani za kishirikiana hivyo amewaomba viongozi wa dini kuuombea mkoa huo ili
mauaji hayo yaishe.

Katika
hatua nyingine amesema jamii bila kumtegemea mwenyezi Mungu ni ngumu kuacha
matendo maovu hivyo taasisi za dini zina jukumu hilo na iwapo wakiamua
inawezekana kabisa binaadamu wanaishi kwa amani bila kutendeana matendo
mabaya.
Kwa
upande wake kiongozi wa kanda ya Magaribi wa kanisa hilo mchungaji Wisdom
Shangwe amesema wametoa Msaada wa matairi hayo yenye thamani ya shilingi
2,100,000 ili kulisaidia jeshi la katika kutekeleza majukumu yake.
Amesema
hivi sasa lengo la kanisa hilo ni kusaidiana na serikali katika
kuwasaidia vijana waachane na maovu pia waache kutumiwa na baadhi ya wanasiasa wasio
na nia njema ambao wamekuwa wakiwatumia vijana kwa maslahi yao binafsi.
Wakati
huo huo,ameahidi kuendelea kuuombea mkoa wa Rukwa pamoja na taifa kwa ujumla
sambamba na viongozi wa serikali ili waendelee kumtumainia mwenyezi Mungu
wakati wanapotekeleza majukumu yao.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments