ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 11 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA MANISPAA YA MPANDA

Jengo la Ofisi za Manispaa ya Mpanda na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Na.Issack Gerald-Katavi
Zaidi ya shilingi bilioni 11,750,000,000  zimetengwa kwa ajili ya kuboresha barabara katika Halmashauri ya Manispaa ya  Mpanda Mkoani Katavi.

Hatua hiyo imeelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya  Manispaa ya  Mpanda Enelia  Lutungulu wakati wa   mkutano  wa wadau  wa  mpango  kabambe wa Master   plan ya miaka 20.
Lutungulu amesema fedha hiyo ni mpango wa uboreshaji miundombinu  ya Manispaa uitwao ULGSP uliopangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano ambapo miradi saba imepangwa kutekelezwa katika halmashauri 18 hapa nchini. 
Aidha Lutungulu amesema  mpango wa  uboreshaji wa   miundo mbinu katika  Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda  ulianza  tangu mwaka wa fedha wa  2013/2014 na  utakamilika mwaka wa fedha wa 2017 na2018.
Lutungulu  ameitaja  miradi saba iliyopangwa kutekelezwa  kwenye mradi huo kuwa ni usanifu wa miradi ya barabara na ujenzi wa  soko la kisasa katika Kata ya Kazima, ujenzi wa Stendi ya  mabasi ya  kisasa katika  eneo la  Ilembo, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha  lami zenye urefu wa kilometa 7.7  Mpanda Mjini na uandaaji wa mpango  kabambe  wa  Manispaa ya  Mpanda na kujenga uwezo.
Mradi huo  utatekelezwa na  mtaalamu mshauri  City Plan Consultancy T Limeted kwa gharama ya shilingi za
kitanzania 283 600,000  Fedha  ambazo zimetolewa na Manispaa ya  Mpanda  kupitia  mpango wa utekelezaji wa miji  unaofdhiliwa kwa  mkopo wa  Benki ya Dunia.
Afisa  Mipango  miji  mshauri  wa  City Plan   Consultancy T  Limeted ya Dar es salaam Bw.Iddy  Mwerangi   alisema ni lazima ziunganishwe nguvu   za wadau  mbalimbali zitakazosaidia   kupatikana  kwa taarifa  mbalimbali zitakazowezesha uaandaaji  wa  mpango Kabambe.
Naye Makamu Meya wa Manispaa ya  Mpanda John   Matongo alisema swala  hilo   bila  ushirikiano wa wananchi  haliwezi kufanikiwa  hivyo  wao  kama madiwani  watahakikisha  zoezi  hilo la  mpango Kabambe wa  Master   Plan  linafanikiwa.
Kwaupande wake mkuu  wa  mkoa  wa  Katavi   Meja Jenerali   mstaafu   Raphael   Muhuga  alisema  kuwa  mji wa  Mpanda  unakuwa  kwa  hivyo ni vema  maeneo ya mji huo  yakawa  yamewekwa  kwenye  mpango unaoeleweka.
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ni miongoni mwa halmashauri hapa nchini zinazotekeleza miradi inayofadhiliwa na benki ya dunia ambapo pamoja na Miradi mingine Halmashauri ya manispaa ya Mpanda inaandaa mpango kabambe maarufu kama Master Plan utakaoongoza matumizi ya ardhi ya manispaa ya Mpanda kwa kipindi  miaka 20 ijayo.
Mpango mchakato huo uliokuwa umeanza tangu mwaka 2010, haukufika mwisho kwa sababu ya ongezeko la mahitaji ikiwa ni pamoja na ongezeko la ukubwa wa eneo la kiutawala manispaa ya Mpanda hivyo kupelekea kuanza upya Mchakao huo kwa kuwa taarifa za awali za msingi zilipitwa na muda wake.
Kwamujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Manispaa hiyo ilikuwa na jumla ya wakazi 102,900 hivyo kupelekea kwenye mpango huo kupata  mgao wa  Dola  za kimarekani 7,342,975, ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania 11,750,000,000 ambazo zitatumika kutekelezwa mpango huo kwa  muda wa miaka mitano.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group 


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA