ORODHA KAMILI YA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI WA RAIS MAGUFULI ALILOTANGAZA LEO

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Rais Dkt John Magufuli wa Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli  leo amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kwa kuongeza idadi ya Wizara, kuteua Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya na kuwahamisha Wizara baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri.

Katika mabadiliko hayo Mhe.Rais Magufuli ameongeza idadi ya Wizara na Mawaziri wake kutoka 19 hadi 21, na Naibu Mawaziri kutoka 16 hadi 21.
Iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini imegawanywa na kutakuwa na Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini na iliyokuwa Wizara Kilimo,Mifugo na Uvuvi imegawanywa na kutakuwa na Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mhe.Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa ametangaza mabadiliko hayo Ikulu Jijini Dar es Salaam na lifuatalo ni Baraza la Mawaziri baada ya kufanyiwa mabadiliko.
1.Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora-Waziri –George Huruma Mkuchika
2.Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Waziri  Selemani Said Jafo,Naibu Waziri-Joseph Sinkamba Kandege,Naibu Wazri -George Joseph Kakunda
3.Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Waziri January Yusuf Makamba,Naibu Waziri -Kangi Alphaxard Lugola
4.Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu-Waziri -Jenista Joackim Mhagama,Naibu Waziri Anthony Peter Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira),Naibu Waziri - Stella Alex Ikupa (Walemavu)
5.Wizara ya Kilimo Waziri -Dkt. Charles John Tizeba,Naibu Waziri -Dkt.Mary Machuche Mwanjelwa
6.Wizara ya Mifugo na Uvuvi- Waziri Luhaga Joelson Mpina,Naibu Waziri - Abdallah Hamis Ulega
7.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Waziri  Prof.Makame Mbarawa Mnyaa,Naibu Waziri-Mhandisi Atashasta Justus Nditiye,Naibu Waziri-Elias John Kwandikwa
8.Wizara ya Fedha na Mipango Waziri-Dkt. Philip Isdor Mpango,Naibu Waziri -Dkt. Ashatu Kijaji
9.Wizara ya Nishati-Waziri Dkt.Medard Matogoro Kalemani,Naibu Waziri -Subira Hamis Mgalu
10. Wizara ya Madini-Waziri -Angellah Kairuki,Naibu Waziri -Stanslaus Haroon Nyongo
11.Wizara ya Katiba na Sheria,Waziri-Prof. PalamagambaJohn Aidan Mwaluko  Kabudi.
12. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki-Waziri -Dkt. Augustine Philip Mahiga,Naibu Waziri -Dkt. Susan Alphonce Kolimba
13. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT)-Waziri Dkt. Hussein Ali Mwinyi
14. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi-Waziri              Mwigulu Lameck Nchemba,Naibu Waziri-Mhandisi Hamad Yusuf Masauni
15. Wizara ya Maliasili na Utalii-Waziri-Dkt.Hamisi Andrea Kigwangalla,Naibu Waziri-Josephat Ngailonga Hasunga
16.Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi-Waziri William Vangimembe Lukuvi,Naibu Waziri-      Angelina Sylivester Mabula
17.Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Waziri-Charles Paul Mwijage,Naibu Waziri-Mhandisi Stella Martin Manyanya
18.Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi-Waziri Prof. Joyce Lazaro Ndalichako,Naibu Waziri-William Tate Ole Nasha
19.Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Waziri-Ummy Ally Mwalimu,Naibu Waziri -      Dkt.Faustine Engelbert Ndugulile
20.Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo-Waziri -Dkt. Harrison George Mwakyembe,Naibu Waziri Juliana Daniel Shonza
21.Wizara ya Maji na Umwagiliaji-Waziri Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe,Naibu Waziri - Jumaa Hamidu Aweso
Wakati huo huo,Mhe.Rais Magufuli amemteua Bw. Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya Uteuzi huo,Bw.Stephen Kagaigai alikuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri.
Bw.Stephen Kagaigai anachukua nafasi ya Dkt.Thomas D. Kashilila ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Wateule wote wanatarajia kuapishwa Jumatatu ya Oktoba 9,2017 saa 3:30 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA